Pata taarifa kuu
Ufaransa- Ujerumani-Vita vya kwanza vya dunia

Miaka 96 tangu kusitishwa vita vya kwanza vya dunia

Ni miaka 96 tangu usainiwe mkataba wa usitishwaji vita vya kwanza vya dunia, ilikua Novemba 11 mwaka 1918. Nchi 19 zilishiriki katika vita hivyo vilivyoanza mwaka 1914 hadi mwaka 1918, na kusababisha vifo vya watu milioni 18, wakiwemo wanajeshi na raia wa kawaida. 

Rais Ufaransa, François Hollande atazindua "Mnara wa kumbukumbu" unaojulikana kwa jina la "Notre-Dame-de-Lorette" ambapo majina ya 580,000 ya mashujaa katika vita vya kwanza vya dunia kutoka mataifa mbalimbali yameandikwa kwenye Mnara huo.
Rais Ufaransa, François Hollande atazindua "Mnara wa kumbukumbu" unaojulikana kwa jina la "Notre-Dame-de-Lorette" ambapo majina ya 580,000 ya mashujaa katika vita vya kwanza vya dunia kutoka mataifa mbalimbali yameandikwa kwenye Mnara huo. REUTERS/Pascal Rossignol
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa kwa upande wake, ilipoteza wanajeshi milioni 1.5 pamoja na raia wa kawaida 300,000.

Mkataba wa usitishwaji vita vya kwanza vya dunia ulisainiwa saa 11 na dakika 15 alfajiri Novemba 11 mwaka 1918 kwenye umbali wa kilomita zaidi ya mia moja kusini mwa mji wa Paris, nchini Ufaransa, kati ya majeshi ya Ufaransa na Ujerumani, vita ambavyo vilidumu miaka 4. Mkataba huo ulianza kutekelezwa kwenye uwanja wa mapigano saa 5 za mchana.

Novemba 11 mwaka 1920, Ufaransa ilitoa heshima za mwisho kwa mwanajeshi asiye julikana aliye fariki wakati wa vita vikuu. Mwanajeshi huyo anawakilisha wanajeshi waliouawa na ambao miili yao haikuonekana. Kaburi la mwanajeshi huyo liko katika mji wa Paris.

Miongoni mwa wanajeshi hao milioni 1.5 waliofariki katika vita vya kwanza vya dunia, theluthi tatu ya wanajeshi hao (500,000), hawakutambuliwa. Familia moja kati ya tatu haikufanikiwa kumzika ndugu yake, ambaye alikua miongoni mwa wanajeshi walioshiriki vita vya kwanza vya dunia.

Rais wa Ufaransa, François Hollande, anatazamiwa kutoa heshima kwa wanajeshi hao waliofariki katika vita vya kwanza vya dunia. Sherehe hizo zitafanyika Jumanne asubuhi kwenye Ikulu ya Paris, kabla ya kujielekeza kaskazini mwa Ufaransa, ambako atazindua rasmi Mnara wa kumbukumbu kwa wanajeshi hao. Majina 580,000 ya mashujaa katika vita hivyo kutoka mataifa mbalimbali yameandikwa kwenye Mnara huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.