Pata taarifa kuu
Marekani - Syria

IS lakabiliwa na mashambulizi nchini Syria, Al Nosra yatishia bara la Ulaya na Marekani

Muungano wa nchi zilizo jiunga kupambana na waislam wenye msimamo mkali wa Islamic State unaongozwa na Marekani umeshambulia kituo cha gesi nchini Syria kilichokuwa chini ya udhibiti wa kundi hilo, wakati huu kundi la Alqaeda likitishia kutekeleza mashambulzi katika nchi za magharibi.

ndege za Vikosi vya muungano zikishambulia ngome za IS nchini Syria
ndege za Vikosi vya muungano zikishambulia ngome za IS nchini Syria REUTERS/U.S. Air Force
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na shirika la haki za binadamu nchini Syria, shirika ambalo lipo karibu na upinzani wa nchi hiyo limearifu kuwa kwa mara ya kwanza mashambulizi ya muungano huo yametekelezwa katika kituo cha gesi mashariki mwa Syria katika jimbo la Deir Ezzor karibu na mpaka wa Syria eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Mkurgenzi wa shirika hilo la haki za binadamu nchini SyriaRami Abdel Rahman amesema mashambulizi ya hii leo yamelenga kiwanda cha Coneco kilichokuwa chini ya u

Ramani ya mashambulizi ya Marekani katika ngome za IS nchini Syria
Ramani ya mashambulizi ya Marekani katika ngome za IS nchini Syria

dhibiti wa waasi wa Islamic State. Kulingana na kiongozi huyo lengo hasa ilikuwa ni kuwaondowa wapiganaji hao katika kiwanda hicho, na hakuna aliepoteza mauaji mbali na majeraha ya wapiganaji kadhaa.

Marekani na kundi la nchi kadhaa za kiarabu hususan nchi za ghuba, zimeanza mashambulizi ya anga tangu septemba 23 dhidi ya ngome za wapiganaji wa kundi la Islamic State nchini Syria, ikiwa ni mwezi mmoja na nusu baada ya kutekeleza mashambulzi kama hayo katika nchi jirani ya Iraq.

Lengo hasa la mashambuliz hayo ni kuharibu chanz cha ufadhili wa kundi hilo la kijihadi ambalo linauza mafuta kutoka katika maeneo ambayo linamiliki.

Mashambulizi ya jana jumapili yalilenga viwanda vinne pamoja na kituo cha uongozi wa IS karibu na mji wa Raqa kaskazini mwa Syria, duru za uongozi wa jeshi la Marekani katika ukanda wa mashariki ya kati Centcom, zimedhitbitisha.

Wakati huu mashambulizi ya muungano yakishika kasi, kiongozi wa kundi la Al Nusra, kitengo cha kundi la Alqeda nchini Syria, ametishia kulipiza kisase kupitia mashambulizi ya raia wa nchi za magharibi zilizojiunga na muungano unaonogzwa na Marekani.

Hii ni mara ya kwanza kiongozi wa Al Nosra, Abou Mohammed al- Joulani anazungumza hadharani tangu kuanza kwa mashambulizi dhidi ya kundi la Islamic State.

Katika wito uliorikodiwa na kusambazwa kwenye mtandano wa Internet, kiongozi huyo anawatolea wito waanchi wa Marekani na Ulaya kupinga hatuwa ya serikali zao, na kutishia kuelekeza mshambulizi katika familia zao.

Barack Obama rais wa Marekani
Barack Obama rais wa Marekani REUTERS/Kevin Lamarque

Hayo yanajiri wakati huu Rais wa Marekani Barrack Obama akikiri kuwa, Marekani ilipuuza madhara ambayo yangesababishwa na wapiganaji wa Kiislamu wa Islamic State nchini Syria. Akizungumza na runinga ya CBS, Obama amesema magaidi wa Al Qaeda waliofurushwa nchini Iraq walikimbilai nchini Syria na kuunda kundi la Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.