Pata taarifa kuu
UKRAINE-MAREKANI

Rais wa Marekani Barack Obama akutana na rais mteule wa Ukraine, Petro Poroshenko

Rais wa Marekani Barack Obama akiwa kwenye ziara yake barani Ulaya, hii leo aamekutana kwa mazungumzo na rais mteule wa Ukraine, Petro Poroshenko hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa viongozi hawa kukutana toka nchi ya Ukraine ilipofanya uchaguzi wake mkuu juma moja lililopita.

Rais mteule wa Ukraine, Petro Poroshenko akizungumza na rais wa Marekani, Barack Obama
Rais mteule wa Ukraine, Petro Poroshenko akizungumza na rais wa Marekani, Barack Obama REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Obama ambaye bado yuko mjini Warsaw nchini Poland, amekutana na rais Poroshenko kwenye mazungumzo ambayo rais Obama amemuahidi kiongozi huyo kuwa nchi yake itaendelea kuwa karibu nae na itamsaidia kiusalama.

Kwenye mkutano wao, rais Obama amemuhakikishia usalama na ushirikiano wa nchi yake kwa taifa la Ukraine na kwamba bado nchi yake itaendelea kuwa mshirika wa karibu wa taifa hilo na ukanda wa Ulaya.

Mkutano kati ya rais Obama na rais Poroshenko unafanyika wakati huu ambapo hapo jana alikutana na viongozi viongozi wa Ulaya mashariki na kisha baadae hii leo ataelekea mjini Brussels Ubelgiji kwa mkutano na viongozi wa G7 kwenye mkutano unaolenga kujadili hatau mpya ya Urusi kuhusu kuunganisha mataifa yaliyokuwa kwenye utawala wa Kisoviet.

Rais mteule wa Ukraine, Petro Poroshenko
Rais mteule wa Ukraine, Petro Poroshenko REUTERS/David Mdzinarishvili

Rais Barack Obama atakutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza toka nchi hiyo ilipojiingiza kwenye mzozo wa Ukraine na kulitambua jimbo la Crimea wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya vita ya pili ya dunia "D-Day" itakayofanyika kwenye mji wa Normandy nchini Ufaransa siku ya Ijumaa.

Rais Obama pamoja na viongozi wengine wa Ufaransa, Uingereza na Ujerumani wanatarajiwa kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana na rais wa Urusi Vladmir Putin ambaye nae alialikwa na rais wa Ufaransa, Francois Hollande kuhudhuria sherehe hizo.

Rais wa Marekani Barack Obama akizungumza jana akiwa mjini warsaw nchini Poland
Rais wa Marekani Barack Obama akizungumza jana akiwa mjini warsaw nchini Poland REUTERS/Kevin Lamarque

Akiwa mjini Kiev hapo jana rais mteule, Petro Poroshenko amesisitiza kuwa eneo la Crimea hivi karibuni litarejea kwenye himaya ya nchi hiyo na kwamba hilo hana wasiwasi nalo kwakuwa ameshaanza mazungumzo na viongozi wa Urusi.

Rais Poroshenko ameyasema hayo wakati akitoa tuzo kwa viongozi wa Tata wa eneo la mashariki mwa nchi hiyo ambao wametoa mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa eneo la mashariki mwa nchi hiyo haliendelea kugawanyika.

Rais Poroshenko alisema "Mimi ninaamini bado kuwa eneo la Crimea hivi karibuni litakuwa eneo la Ukraine tena, kwa hili sina wasiwasi nalo kwakuwa ninauhakika nalo". Alisema rais Poroshenko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.