Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI

Hali ya sintofahamu yaendelea kushuhudiwa nchini Ukraine

Hali ya sintofahamu yanedelea kuripotiwa nchini Ukraine wakati huu kukirpotiwa vifo vya zaidi ya watu 30 walipoteza maisha, huku juhudi za kidiplomasia kutafuta suluhusu ya mzozo huo zikishka kasi, na Umoja wa Mataifa ukizitaka pande zote mbili kuweka silaha chini.

Mjumbe wa haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navy Pillay
Mjumbe wa haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navy Pillay
Matangazo ya kibiashara

Mjumbe wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navy Pillay amelaumu machafuko yanayoendelea kushuhudiwa nchini Ukraine, na kutowa wito wa serikali na waasi wanaotaka mjitengo wa eneo la mashariki mwa Ukraine kuwa upande wa Urusi na kusitisha mapigano na kutatua mzozo kwa njia ya Amani.

Navi pillay ameitaka serikali ya Ukraine kuheshimu sheria za kimataifa katika Operesheni zake za kijeshi, na kuwatendea haki wananchi wa Ukraine wanaozungumza lugha ya Urusi.

Kundi la wananchi lilijizatiti kwa silaha nalo limetakiwa kuweka silaha chini, na kuwaacha huru matrka wote linaowashikilia na kuondoka katika ofisi za serikali wanazo shikilia.

Hayo yanajiri wakati huu Spika wa bunge La Urusi Sergueï Narychkine akitahadharisha kuhusu kufanyika kwa mauaji ya kimbari siku moja baada ya kuripotiwa vifo vya watu zaidi ya 30 katika eneo la Slaviansk, huku akikumbusha kuhusu mauaji yaliotkea mei 2 mwaka huu katika mji wa Odessa yaliogharimu maisha ya watu zaidi ya Arobaini.

Kauli hiyo ya Spika wa Bunge la Urusi imetolewa wakati huu juhudi za kidiplomasia kuutuliza mzozo huo wa Ukraine zikishika kasi jijini Vienna ambako wanakutana zaidi ya mawaziri thalathini wa mambo ya nje akiwemo wa Urusi Sergei Lavrov na wa Ukraine Andriï Dechtchitsa kujadili kuhusu mzozo huo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.