Pata taarifa kuu
ITALIA

Idadi ya wahamiaji haramu waliopoteza maisha kisiwani Lampedusa yafikia 232

Wapigambizi nchini Italia wanasema wamepata miili zaidi ndani ya boti lililozama wakati limewabeba wahamiaji haramu kutoka barani Afrika wiki iliyopita wakielekea barani Ulaya katika kisiwa cha Lampedusa nchini Italia.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu miili zaidi ya thelathini ilipatikana na idadi ya watu waliopoteza maisha yao katika ajali hiyo sasa imefikia watu 232 kwa mujibu wa serikali ya Italia.

Hata hivyo, wahamiaji haramu 155 waliokolewa baada ya boti yao kuzama kwa kile wataalam wanasema kuwa chanzo kilikuwa ni kushika moto kwa mitambo ya boti hiyo iliyokuwa na wahamiaji haramu 500 wakitokea nchini Somalia na Eritrea.

Serikali ya Italia imekanusha madai kuwa imekuwa ikifanya uokoaji tarabatibu na tayari serikali ya Ufaransa imetaka kufanyika kwa kikao cha dharura cha Umoja wa Ulaya kujadili suala la ongezeko la wahamiaji haramu wanaokimbilia barani humo.

Italia imesema kuwa itarekebisha sheria za uhamiaji ili kukabiliana na kuingia kwa wahamiaji haramu nchini humo kutokana na idadi yao kuongeza katika siku za hivi karibuni.

Serikali ya Italia inasema kuwa kwa sasa inawashikilia waokoaji ili kuwahoji wahamiaji hao kutoka Eritrea na Somalia na huenda wakachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za Uhamiaji nchini humo.

Mamia ya wahamiaji haramu hukimbilia barani Ulaya kwenda kutafuta maisha mazuri kutokana na hali ngumu ya maisha ya usalama katika nchi zao.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.