Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amsifu Margaret Thatcher kwa kuleta mabadiliko

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amemsifu Kiongozi wa wadhifa wa juu wa zamani nchini Uingereza, Margaret Thatcher ambaye amemsifu kuwa Kiongozi ambaye ameleta mabadiliko makubwa nchini Uingereza.

Waziri mkuu wa uingereza David Cameron
Waziri mkuu wa uingereza David Cameron REUTERS/Chris Radburn/POOL
Matangazo ya kibiashara

Cameron amesema kuwa Thatcher alifungua milango ya mwelekeo wa kisiasa ambayo mpaka sasa inatumika na Uingereza, huku akikosoa wale ambao mtazamo wao umeegemea upande mmoja wa mabaya dhidi yake.

Akiwaga sifa za Marehemu Thatcher, Cameron amesema alichokifanya katika kipindi chake cha uongozi na hata kabla ya kuingia madarakani kilikumbukwa, hasa ukizingati maendeleo alioyaleta katika kuelekea kushikawadhifa wa juu nchini Uingereza

Ingawa baadhi ya wanachama wa Chama cha Labour walikataa kuhudhuria kikao cha Bunge huku wengine wakionesha kutounga mkono siasa zilizokuwa zikiendeshwa na Mwanamama huyu, Kiongozi wa Upinzani Ed Miliband alivunja tofauti hiyo kwa kutambua umuhimu wake kwa Uingereza

Katika hatua nyingine,wakati mipango ya Mazishi ya Margaret Thatcher ikiendelea hali ya usalama iliingia dosari ambapo shamrashamra za kushangilia kifo cha mwanamama huyu kwenye miji kadhaa ziliishia kwa watu kutiwa mikononi mwa Polisi kwa kusababisha vurugu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.