Pata taarifa kuu
SYRIA

Watoto wanaotumikishwa kijeshi kwenye mapigano ya Syria waongezeka

Shirika la misaada la Uingereza limesema idadi ya watoto wanatumikishwa kwenye mapigano nchini Syria imekuwa ikiongezeka kadri siku zinavyokwenda. Shirika hilo limebaini kuwa pande zote mbili zinazokinzana yaani jeshi la waasi na lile la serikali wamekuwa wakiwatumia watoto wa kiume kama wanajeshi katika mapigano yao.

REUTERS/Muzaffar Salman
Matangazo ya kibiashara

Aidha watoto wa kike wamekuwa wakinyanyaswa kingono na wakati mwingine kulazimishwa kuingia katika ndoa wakiwa na umri mdogo.

Katika ripoti yake shirika hilo la Save the Children limesema katika miaka miwili ya machafuko nchini Syria watoto milioni mbili wameathirika na mapigano hayo.

Ripoti hiyo inayoitwa “Children Under Fire” imebaini kuwa kati ya watoto watatu nchini Syria mmoja wao huwa ni muathirika wa unyanyasaji unaotokana na mapigano yanayoshuhudiwa nchini humo.

Mkuu wa shirika hilo Carolyn Miles amesema watoto wengi wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu wakikabiliwa na uhaba wa chakula na dawa wanapokuwa wagonjwa au kujeruhiwa.

Wakati malalamiko hayo yakitolewa pande zote mbili bado hatma ya Taifa hilo haijajulikana baada ya pande zote mbili kutokubaliana juu ya mchakato wa kutafuta amani.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa UN watu zaidi ya elfu sabini wamepoteza maisha tangu yalipozuka mapigano ya kutaka kuuangusha utawala wa Rais Bashar Al Assad mwezi machi mwaka 2011.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.