Pata taarifa kuu
Ufaransa

Maandamano makubwa yafanyika kupinga ndoa za jinsi moja nchini Ufaransa

Maandamano makubwa yameshuhudiwa jana nchini Ufaransa ya watu wanaopinga sheria ihusuyo ndoa ya watu wa jinsi moja lakini pia sheria inayo ruhusu watu wenye jinsi moja kuasili watoto, ambapo muswada wa sheria utajadiliwa bungeni Januari 29 mwaka huu.

REUTERS/Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Vijana ambao wengi ni waumini wa kanisa katoliki wamesema hawajahamasishwa na familia zao kuandamana bali wamekuja kuonyesha kwamba wanapinga sheria hiyo ambayo itawanyima haki watoto kutambulika na kujuwa hasa asilia yao, na kwamba kuwa msagaji au msenge kwao sio kitu .

Wanasiasa kutoka chama tawala cha UMP Jean-François Cope, Mario Marechal Le Pen mbunge wa chama cha FN lakini pia na wabunge kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa nchini humo ambao wanapinga hatuwa ya mtu kuamuwa kuowa watu wawili wenye jinsi moja.

Miongoni mwa waandamanji walikuwemo pia mawakili walioandamana wakivalia sare zao na kusema kwamba wamekuja kuunga mkono haki ya watoto ambayo inaelekea pabaya nchini humo iwapo sheria hiyo itapasishwa na ambayo itawafanya wafaransa wajutie baadae.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.