Pata taarifa kuu
UGIRIKI

Serikali ya ugiriki yasisitiza kuendelea na Mchakato wa Mabadiliko ya kiuchumi ingawa kumekuwa na Upinzani

Ugiriki itaendelea kusimamia katika suala la kufanya Mabadiliko zaidi ya kiuchumi ingawa kumekuwa na pingamizi ndani ya Serikali ya Muungano, Wizara ya Fedha nchini humo imeeleza hii leo

Waziri Mkuu wa Ugiriki, Antonis Samaras
Waziri Mkuu wa Ugiriki, Antonis Samaras REUTERS/Tobias Schwarz
Matangazo ya kibiashara

Mbali na kuwa kumekuwa na hali ya sintofahamu katika muda wa nyongeza ya miaka miwili katika kufikia malengo yake, Vyanzo vya habari vinasema kuwa Mchakato wa kubana Matumizi utaendelea kama ilivyopangwa.
 

Serikali ya Ugiriki imekuwa ikijaribu kwa Miezi kadhaa kukamilisha Mchakato wa kupata namna ya kuokoa kiasi cha Euro bilioni 13.5 wakijadiliana na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya, Shirika la fedha duniani, IMF na Benki kuu ya Ulaya kwa pamoja wajulikanao kwa jina la TROIKA.
 

Ingawa sehemu kubwa ya Makubaliano imefanyika, kumekuwa na Upinzani ndani ya Serikali iliyoundwa kwa Vyama vitatu hasa pingamizi juu ya Nyongeza ya Umri wa kustaafu kama iliyopendekezwa na Mashirika wakopeshaji.
 

Hatua ya pili ya kubana Matumizi na Mabadiliko ya kiuchumi nchini Ugiriki unahitajika ili kupata mkopo wa kitita cha fedha cha Euro bilioni 31.2 .
 

Waziri wa Fedha Yannis Stunaras aliliambia Bunge hapo jana kuwa TROIKA imeridhia kutoa Muda zaidi kwa ugiriki ili iweze kufikia Malengo yake.
 

Lakini Maafisa kutoka Umoja wa Ulaya na IMF wameweka wazi kuwa TROIKA bado haijafikia Makubaliano yeyote na Ugiriki ingawa kumekuwa na maendeleo katika Mazungumzo yao, hata hivyo bado kuna maswala mengine ya kuyaangalia kabla makubaliano.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.