Pata taarifa kuu
MAREKANI-ISRAEL-IRAN

Israel yataka kuchukuliwa hatua zaidi dhidi ya Iran licha ya mataifa sita kutaka kufanyika mazungumzo

Kufuatia maazimio ya nchi sita zenye kura ya turufu kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana kuweka wazi msimamo wao kuhusu Iran na kutaka kufanyika mazungumzo zaidi ya wazi, Serikali ya Israel imesema haikubaliani na mpango huo. 

Rais wa Israel Shimon Peres
Rais wa Israel Shimon Peres Reuters
Matangazo ya kibiashara

Akizungumzia maazimio ambayo yamefikiwa na mataifa Sita ya Ulaya, rais wa Israel Shimon Peres amesema kuwa kwasasa ni lazima vikwazo dhidi ya Iran viongezwe na kwamba kusiwe na mijadala mingi ya wazi kuhusu Iran kwakuwa nchi hiyo imekwishaonywa vyakutosha.

Kiongozi huyo licha ya kusita kuweka wazi endapo nchi yake inampango wa kuivamia kijeshi nchi ya Iran kwa siku za hivi karibuni, lakini kwa upande mwingine imeonekana kuunga mkono hatua ya kurejea kwenye mazungumzo.

Akizungumzia kuhusu muonekano wa Marekani kuhusu msimamo mpya juu ya Iran, Peres amesema kuwa njia zote ziko wazi kwa nchi ya Iran kuachana na mpango wa kurutubisha Uranium.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa mpango wa Iran hivi sasa ni kutaka uungwaji mkono na mataifa ya mashariki ya kati kwa lengo la kutafuta watu ambao wataiunga mkono kutokana na mpango wake.

Hapo jana Umoja wa Mataifa kupitia kwa viongozi wa shirika linalosimamia nguvu za Atomic duniani, walisema kuwa wanaikaribisha Iran kwenye meza ya mazungumzo kuweza kumaliza mzozo uliopo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.