Pata taarifa kuu
URUSI

Waziri mkuu Putin asisitiza kutojiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais hata kama utaingia kwenye duru la pili

Waziri mkuu wa Urusi Vladimir Putin ameendelea kusisitiza kuwa hatojitoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania urais iwapo itatokea kuwa watalazimika kwenda kwenye duru la pili la uchaguzi.

Waziri mkuu wa Urusi Vladimir Putin (kushoto)
Waziri mkuu wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) REUTERS/Alexsey Druginyn
Matangazo ya kibiashara

Akiunukuliwa na kituo cha televisheni ya taifa ya nchi hiyo, waziri mkuu Putin amedai kuwa licha ya kuwa chama chake kinatarajiwa kupata upinzani mkubwa kwenye uchaguzi wa mwezi wa tatu mwaka huu lakini hatojitoa endapo utalazimika kuingia kwenye duru la pili.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa huenda uchaguzi wa mwaka huu nchini humo ukafanyika kwa awamu mbili kwa kile wanachoeleza kuwa ni ushindani ulioonekana wakati wa kura ya maoni ambao umeonsha chama tawala kupoteza umaarufu wake.

Waziri mkuu Putini anaingia kwenye kinyang'anyiro hicho akiwania kupewa muhula wa tatu wa kuongoza taifa hilo mara baada ya kuachia madaraka ya urais wa rais wa sasa Dimitry Medvedev.

Katika hatua nyingine waziri mkuu Putin amewaonya viongozi wa upinzani ambao wanataka kutumia mwanya wa uchaguzi mkuu nchini humo kutaka kuchochea machafuko na kuahidi kuwa vitendo hivyo havitavumiliwa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.