Pata taarifa kuu
Italia

Serikali ya Italia kutangaza hali ya hatari kwenye Pwani ya Tuscan

Serikali ya Italia inatarajia kutangaza hali ya hatari kwenye Pwani ya Tuscan kutokana na kuhofia kuvuja kwa mafuta ya Meli ya Costa Concordia ambayo yatachangia janga la kimazimngira wakati huu msako wa watu ishirini na tisa ukiendelea.

Meli Kubwa iliyopinduka pwani ya magharibi ya  Italia
Meli Kubwa iliyopinduka pwani ya magharibi ya Italia Reuters/Giglionews.it
Matangazo ya kibiashara

Hofu kubwa imeanza kutanda katika eneo la Kisiwa Cha Giglio kutokana na matenki ya mafuta ya meli hiyo kudhaniwa kuwa yameanza kuvuja mafuta huku nahodha Francesco Schettino akiendelea kuhojiwa juu ya ajali hiyo.

Uongozi wa Kampuni inayomiliki meli hiyo imekiri kuwepo kwa makosa aliyayaita ya kibinadamu wakati huu zoezi la kuwaska watu waliopotea likiendelea.

Tume kutoka umoja wa mataifa inayojishughulisha na maswala ya usafiri wa majini huenda ikafanya ikaangalia upya Sheria za kimataifa za usalama wa Meli kubwa za abiria,ili kuepuka ajali kama iliyotokea nchini Italia
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.