Pata taarifa kuu
UTURUKI

Uturuki yasitisha uhusiano wa kibalozi na kijeshi na nchi ya Ufaransa

Nchi ya Uturuki imetangaza kusitisha uhusiano wa kibalozi na taifa la Ufaransa kufuatia hatua ya wabunge wa nchi hiyo kupiga kura kukataa nchi yao kuhusika na mauaji ya halaiki ya raia wa Armenia yaliyotokea mwaka 1915.

Waziri mkuu wa Uturuki Racep Tayyip Erdogan
Waziri mkuu wa Uturuki Racep Tayyip Erdogan Reuters
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo wa nchi ya Uturuki umetangazwa na waziri mkuu wa Racep Tayyip Erdogan aliyekiita kitendo cha wabunge la Ufaransa kuwa ni chaunyanyasaji, chaubaguzi wa rangi na kukimbia majukumu ambayo nchi hiyo ilipaswa kuyachukua kuwalipa fidia wananchi walioathirika na mauaji hayo.

Hapo jana bunge la Ufaransa lilipitisha sheria mpya ambayo itayabana mataifa ambayo yalihusika na mauaji ya warmenia kutokataa kuhusika kwao, hii ikiwa na maana kuwa nchi ya Uturuki chini ya utawala wa Ottoman ilihusika na mauaji hayo ya wakati wa vita ya kwanza ya dunia.

Waziri mkuu Erdogan amesema kuwa nchi yake haikubaliani na hatua hiyo ya Ufaransa na kusisitiza kuwa nchi yake haikuhusika na mauaji hayo kamwe na kwamba inapitia upya uhusiano wake na nchi ya Ufaransa.

Nchi ya Uturuki imeendelea kuilaumu Ufaransa kwa kupitisha sheria hiyo ikisema kuwa kamwe historia haiwezi kufutika na kwamba kila mmoja wao aliwajibika katika mauaji ya rais wa Armenia zaidi ya milioni moja na nusu waliouawa kwenye vita hivyo.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Alain Juppe ameelezea kusikitishwa na hatua hiyo ya Uturuki akitaka nchi hizo mbili kufanya mazungumzo kutatua mgogoro unaofukuta.

Nchi ya Ufaransa inwahifadhi zaidi ya raia Laki tano wa Armenia ambo wamepatiwa uraia wa nchi hiyo na ndio wanaoelezwa kumuunga mkono rais wa sasa Nikolas Sarkozy.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.