Pata taarifa kuu
ITALIA

Waziri Mkuu mpya wa Italia ashinda kura ya kuwa na imani naye

Waziri mkuu wa Italia Mario Monti ameshinda kura ya kuwa na imani naye ama la iliyopigwa na bunge la seneti na hivi sasa inaelezwa kuwa ana kibarua cha kufanyia kazi mabadiliko ya kiuchumi ili kutoa matumaini mapya kwa Raia wa Italia.

Reuters/Tony Gentile
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia hali hiyo Umoja wa Ulaya umeunga mkono hatua zitakazochukuliwa na Italia katika kupambana na mzigo wa madeni na kuyumba kwa uchumi hali inayozikabili nchi za Ulaya.

Bunge la seneti liliunga mkono serikali ya Monti kwa kura 281 kati ya 307 za maseneta na kuunga mkono mpango wa kulinusuru taifa hilo kiuchumi.

Akihutubia bunge hilo kwa mara ya kwanza, Monti alitangaza kuwa mpango wa kubana matumizi ni muhimu ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na usawa ikiwemo kuwekeza kwa ajii ya wanawake na vijana.

Monti amewatoa wasiwasi raia wa Italia kwa kuwahakikishia kuwa mabadiliko hayo hayajatokana na msukumo wowote au shinikizo la mataifa ya kigeni.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.