Pata taarifa kuu
UTURUKI

Serikali ya Uturuki yaomba msaada kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya EU

Serikali ya Uturuki imeuomba Umoja wa Ulaya EU msaada wa haraka kwa ajili ya kuwasaidia maelfu ya waathirika wa tetemeko la ardhi ambalo lilipiga nchi hiyo siku ya jumapili likiwa na ukubwa wa saba nukta mbili.

REUTERS/Stringer/Turkey
Matangazo ya kibiashara

Tetemeko hilo la ardhi limesababaisha vifo vya watu wanaokadiriwa kufikia mia tano na thelathini huku wengine elfu moja na mia tatu wakijeruhiwa na wengine maelfu kupoteza makazi.

Tume ya Umoja wa Ulaya EU ndiyo ambayo imetangaza ombi la serikali ya Uturuki kwa nchi zake wanachama ambapo wanatakiwa kutoa msaada wa haraka ili kuweza kusaidia maelfu ya watu wanaohitaji huduma kwa sasa.

Mkuu wa Tume ya Mgogoro ya Ulaya Kristalina Georgieva amesema Mamlaka nchini Uturuki imeomba EU nayo kuungana na Shirika la Mwezi Mwenduku na watu wanaojitolea katika kuhakikisha inawafikia waathirika.

Ombi hilo la serikali ya Uturuki limeanza kujibiwa na nchi wanachama sita zikiwemo Austria, Ubelgiji, Uingereza, Ufaransa, Slovenia na Sweden ambazo zimetoa jumla ya mahema maalum ya kuzuia baridi yapatayo elfu moja na mia mbili kwa wathirika.

Utafiti ambao umefanyika hadi sasa unaonesha kuwa majengo elfu mbili na mia mbili yameharibiwa Kusini Mashariki mwa nchi ya Uturuki baada ya kukumbwa na tetemeko la ardhi siku ya jumapili.

Umoja wa Ulaya EU na Uturuki kwa miaka kadhaa sasa wameendelea kufanya mazungumzo ya kuangalia ombi la serikali ya Ankara kupatiwa uanachama wa Umoja huo wenye wanachama kumi na saba kwa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.