Pata taarifa kuu
Uingereza

Serikali ya Uingereza yaanza kuchukua hatua dhidi ya machafuko

Jeshi la Polisi nchini Uingereza limeanza uchunguzi kifo cha raia mmoja aliyeuawa wakati akijaribu kuzima moto katika Mji wa Liverpool huku wakiwa na picha za Kamera ya CCTV zikionesha kundi hilo la vijana wakimpora na hata kumjeruhi.Β 

(REUTERS)
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi huu unakuja baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kusema Bungeni serikali yake itachukua hatua zote kukabiliana na machafuko ya vijana hao ambao amesema yalikuwa na lengo la uporaji.

Waziri Mkuu Cameron amesema nyuma ya ghasia hizo hakuna msukumo wa kisiasa na wala si maandamano bali ni vitendo vya uporaji ambavyo vimeandaliwa na kufanwa na vijana hao ambao ameahidi kuwasaka.

Β 

Β 

Β Wakati huo Jeshi la polisi nchini Uingereza limekiri kuwa mbinu walizotumia askari wake katika kukabiliana na machafuko yanayoendelea nchini humo zilikuwa dhaifu na hazikuwa sahihi.

β€œMkuu wa polisi amekuwa mkweli na muwazi kwangu kuwa polisi walilichukulia suala hilo kama dogo la kijamii lakini dhahiri suala hilo lilikua ni la kihalifu”, amesema Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron.

Katika hatua nyingine Serikali ya Uingereza imetangaza hatua itakazochukua kuwasaidia wamiliki wa nyumba zilizoharibiwa na wanaotuhumiwa kufanya uhalifu huo.
Aidha Serikali hiyo imetangaza kuwasaidia wafanyabiashara ambao mali zao zimeharibiwa na kuporwa kufuatia machafuko hayo yanayofanyika katika baadhi ya miji ya Uingereza.
Waziri Mkuu Cameron aliweka bayana hatua hizo wakati akihutubia bunge la dharura lililoitishwa leo kwa ajili ya kujadili hali hiyo na hatua za kuchukua katika kukabiliana na vurugu hizo.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron machafuko yalikuwa ni uhalifu wa wazi lakini polisi walikuwa wachache katika mitaa ya maeneo yaliyokumbwa na machafuko na vurugu.
β€œMachafuko hayo ni uhalifu wa wazi lakini polisi hawakutumia mbinu za kufaa kukabiliana na uhalifu huo”, alisema Cameron.
Mpaka sasa watu wapatao 3000 tangu kuanza kwa vurugu hizo mwishoni mwa juma lililopita na watakaokutwa na hatia serikali ya nchi imeapa kuwashughulikia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.