Pata taarifa kuu
Ufaransa

Binti wa Strauss-Kahn ahojiwa kuhusu kesi ya baba yake

Wachunguzi nchini Ufaransa, wamemhoji mmoja wa mabinti za Dominique Strauss-Kahn, kuhusiana na tuhuma za kujaribu kumbaka mwandishi wa habari Tristane Banon.

Dominique Strauss-Kahn,na hakimu  Benjamin Brafman
Dominique Strauss-Kahn,na hakimu Benjamin Brafman Reuters
Matangazo ya kibiashara

Camille Strauss-Kahn amehitimu katika Chuo Kikuu cha Columbia na ni rafiki ya Banon, ambaye anadai kuwa mkuu huyo wa zamani wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), alimdhalilisha kijinsia, mwaka 2003 wakati akimhoji.

DSK anakabiliwa na kesi nyingine kama hiyo, jijini New York Marekani, akituhumiwa kujaribu kumbaka mfanyakazi mmoja wa hoteli huko Manhattan.

Kahn aliyekuwa na matarajio ya kugombea urais mwakani, amekana mashtaka yote na uchunguzi bado unaendelea.

Francois Hollande mgombea wa chama cha wa Socialist nchini Ufaransa kwa uchaguzi wa awali kuelekea uchaguzi wa urais wa mwaka 2012 nchini Ufaransa nae atahojiwa na polisi ya Ufaransa. Wachnguzi wa kesi ya Dominique Strauss-Kahn dhidi ya muandishi habari Tristane Banon kuhusu unyanyasaji wamesema anatakiwa kutokwa mwanga kuhusu kesi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.