Pata taarifa kuu
Uingereza

Gazeti la The News of the World lafungwa kufuatia kashfa ya wizi wa taarifa kupitia mtandao

Kufuatia kashfa ya wizi wa taarifa kwa kutumia mtandao na kuchapishwa kwenye gazeti la The News of the World, mkurugenzi wa gazeti hilo James Murdoch ametangaza kulifunga rasmi gazeti hilo.

James Murdoch mkurugenzi mkuu wa gazeti la The News of the World
James Murdoch mkurugenzi mkuu wa gazeti la The News of the World rfi
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyosomwa na mwakilishi wa mkurugenzi huyo, imesema kuwa siku ya jumapili ya tarehe 10 gazeti hilo litatoa chapisho lake la mwisho na kufunga ofisi zake mjini london.

Mudoch katika taarifa yake amewaomba radhi ndugu na jamaa ambao wameathirika na kuchapishwa kwa taarifa zao na gazeti hilo na kuongeza kuwa anajutia kitendo hicho na ndio maana anaomba radhi kwa yaliyotokea.

Juma hili bunge la uingereza lilikuwa katika mjadala mzito kuhusu taarifa za kuuawa kimakosa kwa wanajeshi wake nchini Iraq na kumshinikiza waziri mkuu David Cameron kuchukua hatua dhidi ya gazeti hilo.

Kufuatia tangazo la mkurugenzi wa the News of the world, wafanyakazi wa gazeti hilo wamepanga kuandaman hii leo kupinga hatua ya kufungwa bila kujua hatma yao itakuwaje.

Hapo jana waziri mkuu wa david Cameron aliahidi jana kuwa uchunguzi wa umma utafanywa kuhusu kashfa hiyo lakini upinzani unasema inavyoonekana serikali haitilii maanani swala hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.