Pata taarifa kuu
Uturuki - Israel

Uturuki na Israel washindwa kuafikiana kuhusu mauaji yaliotekelezwa na makomandoo wa Israel

Nchi za Israel na Uturuki kwa mara nyingine tena wameshindwa kukubaliana kutia saini kwenye taarifa ya mauaji ya wanaharakati tisa wa Uturuki waliouawa na makomandoo wa Israel walipovamia meli ya Flotilla iliyokuwa ikielekea ukanda wa Gaza mwaka mmoja uliopita.

Bendera ya Uturuki
Bendera ya Uturuki Afriquinfos
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa nchi zote mbili wamekataa kutia saini kwenye ripoti ya uchunguzi uliofanywa na umoja wa mataifa huku kila upande ukionyesha kutoridhishwa na ripoti hiyo ambayo inatarajiwa kukabidhiwa kwa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon muda mchache ujao.

Mjumbe toka nchini Uturuki amesema kuwa nchi yake hairidhishwi na ripoti hiyo wakiendelea kuhoji kwanini makomandoo wa nchi hiyo awali walitumia nguvu wakati wa kuisimamisha meli hiyo.

Israel yenyewe ilikataa kutia saini katika ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa baada ya kuhitimisha ripoti yake kwa kuwataja makomandoo wa nchi hiyo kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa operesheni yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.