Pata taarifa kuu
LONDON

Wafanyakazi nchini Uingereza kufanya mgomo wa nchi nzima Alhamisi hii

Wafanyakazi zaidi ya laki sita nchini Uingereza wamedhibitisha kushiriki katika maandamano ya nchi nzima yaliyopangwa kufanywa siku ya alhamisi kupinga mpango wa serikali wa kuongeza muda wa kufanya kazi na nyingeza katika kuchangia mfuko wa Pensheni.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron Reuters/Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Mgomo huo wa nchi nzima ambao utajumuisha waalimu na wafanyakazi wa sekta nyingine umeitishwa na umoja wa vyama vya wafanyakazi zaidi ya vitatu nchini humo wakitaka serikali kubadili uamuzi wa kurekebisha muda wa masaa ya kazi na kuongezewa malipo ya kuchangia mfuko wa pensheni.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, siku ya jumanne alitumia muda wa hotuba yake kuwashawishi wafanyakazi hao kutofanya mgomo huo akisema mabadiliko ambayo yamefanywa na serikali ni yalazima ili kuongeza pato la serikali.

Endapo maandamano hayo yatafanyika yatakuwa ni maandamano makubwa zaidi kuwahi kufanywa nchini humo tangu kuundwa kwa serikali ya umoja inayoongozwa na waziri mkuu Cameron.

Katika hotuba yake waziri mkuu Cameron amewataka viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini humo kuendelea na mazungumzo na serikali kuangalia namna ya kuweza kutatua mgogoro ambao umeibuka mara baada ya kutangazwa kwa sera hiyo mpya ya serikali.

Mpango huo mpya wa serikali, umeongeza muda wa kustaafu kwa miaka sita zaidi ambapo sasa mtu atastaafu akifikisha miaka 66 na kuongeza ajira kwa asilimia hamsini huku muda wa kufanya kazi ukiongezwa kitu kinachopingwa na wafanyakazi.

Wananchi zaidi ya laki tatu na elfu thelathini hawana ajira nchini humo huku serikali ya waziri mkuu Cameron ikiendelea na mpango wake wa kubana matumizi hadi mwaka 2015 ili kukabilina na hali ngumu ya uchumi iliyopo duniani kwasasa.

Mpango huo wa serikali umekuwa ukikosolewa na upinzani pamoja na vyama vya wafanyakazi nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.