Pata taarifa kuu
Ugiriki

Waziri mkuu wa Ugiriki mbioni kuunda serikali mpya

Waziri Mkuu wa Ugiriki, George Papandreou anasema yuko katika harakati za kuunda serikali mpya kama njia mojawapo ya kutafuta uungwaji mkono kutoka umoja wa ulaya na shirika la fedha dunia IMF, ili kulikwamua taifa hilo katika hali ngumu ya kiuchumi.

Waziri mkuu wa Ugiriki George Papandreou
Waziri mkuu wa Ugiriki George Papandreou REUTERS/John Kolesidis
Matangazo ya kibiashara

Leo Alhamisi, Waziri Mkuu Papandreou anatarajiwa kuomba uungwaji mkono bungeni ili kufanya mabadiiko hayo, huku ikioneka kuwa huenda akakumbana na wakati mgumu kutoka kwa chama cha socialist Pasok .

Ghasia zilizuka jana jijini Athens kati ya waandamanaji na polisi katika harakati zao za kuonyesha kusikitishwa na hali ya kiuchumi inavyo didimia nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.