Pata taarifa kuu
UJERUMANI-ULAYA

Serikali ya Ujerumani karibuni kufahamu chanzo cha bakteria wa E.coli

Wataalamu nchini Ujerumani wamefanikiwa kubaini shamba moja lililoko kaskazini mwa nchi hiyo kama eneo ambalo wanahisi bakteria wa E.coli waliobainika kwenye matango na kusababisha vifo vya watu 22 ndiko ugonjwa huo ulipoanzia.

Picha: wananchi wakinunua matunda yanayoshukiwa kuwa yalikuwa na bakteria wa E.coli
Picha: wananchi wakinunua matunda yanayoshukiwa kuwa yalikuwa na bakteria wa E.coli Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wataalamu hao wa magonjwa ya mlipuko wamesema kuwa tayari wamefanikiwa kuchukua sampuli kutoka katika shamba hilo lililoko eneo la mji wa Uelzen na kwamba sasa wanafanyia utafiri ili kupata uthibitisho zaidi.

Waziri wa kilimo nchini Ujerumani juma hili alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa serikali inaendelea na jitihada za utafiti wa chanzo cha bakteria hao na kudai kuwa wameshabaini eneo ambalo wanahisi ugonjwa huo ndiko ulipoanzia.

Waziri huyo ameongeza kuwa wameamua kulifanyia utafiti shamba hilo ambalo amelitaja kuwa moja ya eneo maarufu la kilimo ambapo mbegu zake wanazotumia kuzalisha matunda zinatoka katika mataifa mbalimbali duniani.

Bakteria hao wameelezewa kuwa mara nyingi wanatokea katika mashamba ambayo eneo lake linakadiriwa kuwa na nyuzi joto 30 joto ambalo linachangia bakteria hao kuweza kuishi kwa muda mrefu na kujishika katika matunda.

Tangu kuzuka kwa bakteria hao wa E. coli watu 22 wamedhibitishwa kufa huku zaidi ya watu 2,150 wakielezwa kuathirika kutokana na kula matango hayo yanye bakteria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.