Pata taarifa kuu
London, Uingereza

Obama, Cameron wazungumzia Israeli, Palestina, Libya

Rais wa Marekani Barack Obama na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron wamekutana jijini London nchini Uingereza na kusisitiza kuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi lazima aondoke madarakani.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wamesema kuwa kuondoka kwa Gaddafi kutasaidia kujenga Libya mpya na wanaendelea na jitihada zao za kulinda raia wa nchi hiyo na kuhakikisha demokrasia inashika mkondo wake.

Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari viongozi hao pia wamezungumzia hali ya mgogoro wa Israeli na Palestina na kuelezea hatua wanazochukua katika kushughulikia mgogoro huo.

Hata hivyo wachambuzi wa mambo wamekuwa wakihoji kwa nini viongozi hao wanatoa kipaumbele zaidi katika mgogoro wa Libya na wengine kudai kuwa mafuta ndiyo chanzo cha kutaka kuondoka madarakani kwa Gaddafi.

Kuhusu uhusiano kati ya Marekani na Uingereza Obama na Cameron wamesema kuwa uhusiano wao ni maalum na una nguvu kuliko ilivyowa hi kuwa hapo awali.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.