Katika makala haya utasikia vijana wajasiliamali wakizungumzia namna sekta hiyo inavyoweza kusaidia kukuza uchumi katika mataifa yanayoendelea, karibu
Vipindi vingine
-
Hofu kwa wafanyabiashara kuhusu muswada wa fedha 2024 nchini Kenya
Msikilizaji kwa wiki kadhaa sasa nchini Kenya, kumekuwa na mjadala mkali baada ya kutolewa kwa mapendekezo ya serikali kuhusu muswada wa fedha wa mwaka 2024 unaolenga kuongeza kodi katika baadhi ya sekta na bidhaa nchini humo.Wazalishaji na wawekezaji wakitarajiwa kuwa waathiriwa wakbwa ikiwa muswada huu utapitishwa kama ulivyo, ambapo baadhi ya vinavyolalamikiwa na wazalishaji ni nyongeza ya ushuru wa thamani katika malighafi kutoka nje pamoja na tozo za mazingira maarufu kama Eco Levy.29/05/202410:05 -
Afrika na jitihada za kutaka kuwa katika meza ya majadiliano ya kidunia na sio mualikwa
Msikilizaji wakati wa kongamano la kimataifa la wakurugenzi wakuu wa kampuni mbalimbali duniani waliokutana nchini Rwanda, maswali kadhaa yaliibuliwa, kubwa lilikuwa ni je bara la Afrika linapaswa kuwa katika meza ya maamuzi au kwenye orodha, na ikiwa huu ni muda muafaka wa kutoa mustakabali wake.22/05/202410:02 -
Changamoto na fursa kwa vijana wajasiriamali na ajira kwenye nchi za Afrika Mashariki
Hujambo msikilizaji wa rfikiswahili popote pale unapotegea sikio matangazo yetu nikukaribishe katika makala ya Gurudumu la Uchumi, na hivi leo tunaangazia ukanda wa Afrika Mashariki, eneo lililojaa nguvu kazi ya vijana pamoja na ari ya ujasiriamali, lakini bado linakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira.15/05/202409:58 -
Mchango wa biashara ndogondogo na kati kwa uchumi wa nchi za Afrika Mashariki
Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, inaangazia mchango na changamoto ya biashara ndogondogo na zile za kati kwenye nchi za Afrika Mashariki.Matayarishaji amezungumza na wafanyabiashara wadogowadogo na kati nchini Kenya, lakini mchambuzi wa masuala ya uchumi Ally Mkimo.10/05/202408:14 -
Afrika na madai ya mabadiliko katika mifumo ya kifedha ya kimataifa
Msikilizaji katika miaka ya hivi karibuni, wito umeendelea kutolewa na mataifa ya Afrika kuhusu kuwepo usawa na haki katika mfumo wa kifedha duniani, ambao Kihistoria, nchi za Kiafrika zimekuwa katika hali mbaya linapokuja suala la kupata ufadhili, rasilimali, na makubaliano yenye usawa ya kibiashara.Kuzungumzia hili, nimemualika kwa njia ya simu kutoka Tanzania, Walter Nguma, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara.01/05/202409:40