Pata taarifa kuu
Gurudumu la Uchumi

Afrika na changamoto ya biashara huria kati ya mataifa

Imechapishwa:

Msikilizaji wa rfikiswahili, viongozi wa bara la Afrika kwa miaka kadhaa wamekuwa kwenye harakati za kuhakikisha uchumi wa bara hili unakua kwa haraka na kutoa ushindani wa kibiashara kwa nchi zilizoendelea kama vile Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, Amerika na Asia lakini changamoto zimekuwa nyingi.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mwaka 2012 marais wa Afrika walikutana mjini Addis Ababa, Ethiopia na kukubaliana kuanzisha mchakato wa kuwa na ukanda wa biashara huria, mkakati ambao utashuhudia wananchi wa mataifa haya wakifanya biashara kwa uhuru kwenye nchi zote za bara hili.

Lakini toka kuanzishwa kwa mchakato huu, kumekuwa na chanamoto nyingi ikiwemo Jumuiya zilizopo kutokamilisha baadhi ya mikataba waliyokubaliana kwa wakati, huku wananchi wengi wakionekana kutokujua fursa ambazo wanaweza kuzipata wakifanya biashara wenyewe kwa wenyewe pamoja na kuuza sana nje ya nchi.

Mtangazaji wako hii leo, anazungumza na Dr Honsety Ngowi mtaalamu wa masuala ya uchumi akiwa jijini Dar es Salaam kuangazia hatua hii.

Vipindi vingine
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.