Pata taarifa kuu
Gurudumu la Uchumi

Zaidi ya bilioni 200 hupatikana kila mwaka kutokana na uharibufu wa kimazingira na biashara haramu

Imechapishwa:

Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili imeangazia mkutano wa kimazingira unaofanyika nchini Kenya, mkutano ambao umewakutanisha wadau mbalimbali wa kiuchumi na kimazingira.

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano wa mazingira mjini Nairobi nchini Kenya
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano wa mazingira mjini Nairobi nchini Kenya RFI
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na mazingira UNEA limetoa ripoti ya mwaka ikionesha kuwa zaidi ya dola bilioni 286 hupatikana kila mwaka kutokana na uhalifu wa kimazingira ikiwemo uvunaji wa misitu na uwindaji haramu wa Tembo na Vifaru.

Biashara hii imeelezwa kushamiri kwenye mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki, magharibi na kaskazini mwa Afrika, jambo ambalo linatishia uwepo wa baadhi ya misitu na wanyama pori ambao wamekuwa kivutio cha utalii.

Mtangazaji wa makala hii amezungumza na profesa Vedasto Ndibalema mhadhiri katika chuo cha kilimo cha Sokoine SUA kilichopo mkoani Morogoro.

Vipindi vingine
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.