Pata taarifa kuu
Gurudumu la Uchumi

Jumuiya ya kimataifa yaungana kupambana na uwindaji haramu wa Tembo na Faru

Imechapishwa:

Juma hili kwenye makala ya Gurudumu la Uchumi tumejadili kuhusu harakati za dunia hivi sasa katika kupambana na uwindaji haramu wa tembo na faru ambapo wanyama hawa wameendelea kuuawa na kutishia kutoweka kabisa.

Rais wa Tanzania akipokea msaada wa magari kwaajili ya kupambana na uwindaji haramu
Rais wa Tanzania akipokea msaada wa magari kwaajili ya kupambana na uwindaji haramu Ikulu Tanzania
Matangazo ya kibiashara

Mtangazaji wa makala hii, amezungumza na wadau mbalimbali wa utalii na ambao wanaungana katika harakati hizi za kupiga vita uwindaji haramu wa Tembo na Faru ambao wanazidi kutoweka kutokana na kuwindwa kiholela.

Picha Zaidi

Kwa takriban miaka miwili iliyopita, jumuiya ya kimataifa iliungana na kutangaza vita dhidi ya watu na viongozi ambao wanashiriki kwenye biashara haramu ya uuzaji wa pembe za ndovu na kusafirisha kwenye mataifa ambayo yanahitaji bidhaa hizi.

Mfano nchini Tanzania, inakadiriwa kuwa sasa tembo waliobaki kwenye mbuga mbalimbali nchini humo wanafikia elfu 13 ukilinganisha na miaka ya tisini ambapo walikuwa zaidi ya laki moja.

Kukithiri kwa uwindaji haramu kwenye nchi za Afrika, ndiko kumepelekea nchi hizi kuungana ili kukabiliana na wawindaji haramu ambao wanabadili mbinu zao kila uchao.

Juma hili nchi ya Tanzania ilitia saini mkataba wa ushirikiano na shirika la ICCF katika kuendesha harakati za mapambano dhidi ya uwindaji haramu.

Katika hatua nyingine wizara ya maliasili na utalii nchini Tanzania pia imeanzisha kitengo maalumu cha mamlaka ya wanyama pori Tanzania, TAWA lengo likiwa ni kukipa kitengo hichi nguvu ya kukabiliana na uwindaji haramu wa tembo na faru.

Taarifa zaidi ziko kwenye mtandao wa wizara ya maliasili na utalii ya Tanzania.

Vipindi vingine
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.