Pata taarifa kuu
Gurudumu la Uchumi

Maiaka 50 ya Muungano wa Tanzania

Imechapishwa:

Mtangazaji wa makala hii juma hili amezungumzia kuhusu miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao baadae ulizaa taifa la Tanzani. Tunajadili ni kwa kiasi wananchi wa Taifa hilo wamenufaika kiuchumi ndani ya miaka hii 50 ya Muungano?

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete akikagua gwaride maalumu wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya muungano
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete akikagua gwaride maalumu wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya muungano Ikulu/Issa Michuzi
Matangazo ya kibiashara

Mtangazaji wa makala haya amezungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wataalamu wa masuala ya Uchumi, wabunge na wananchi wa kawaida ambao wanaishi kwenye Jamhuri ya Muungano.

HISTORIA YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa mnamo tarehe 26 Aprili, 1964 kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja).

Tanganyika ilikuwa ni mwendelezo wa koloni la Ujerumani, utawala wa Waingereza kwa Mamlaka ya Umoja wa Mataifa, Himaya ya Umoja wa Mataifa chini ya utawala wa Uingereza na mwisho Taifa huru kuanzia mwaka 1961 ndani ya nchi za Jumuiya ya Madola.

Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ziliingia mkataba wa Muungano mnamo mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkataba huu wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume tarehe 22 Aprili 1964 huko Zanzibar. Mkataba huo ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi hapo tarehe 26 Aprili, 1964 na mnamo tarehe 27 Aprili, 1964, viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam na kubadilishana Hati za Muungano. Sheria za Muungano zilitoa tamko la Jamhuri ya Muungano katika Ibara ya 4 kwamba:

“Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitalazimika, baada ya kuungana na siku zote baada ya kuungana, kuunganishwa kuwa Dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar’ (Ibara ya 4 Sheria za Muungano)

Jina hili la “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar” lilibadilishwa baadae mnamo tarehe 28 Oktoba, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Sheria ya Jamhuri ya Muungano, Sheria namba 61 ya mwaka 1964.

Vipindi vingine
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.