Pata taarifa kuu

Israel: Wapalestina 'karibu 300,000' wameondoka Rafah tangu Jumatatu Mei 6

Jeshi la Israel limetangaza siku ya Jumamosi kwamba "takriban Wapalestina 300,000" wameondoka katika vitongoji vya mashariki vya Rafah, kwenye ukingo wa kusini wa Ukanda wa Gaza, tangu kutolewa agizo la wakaazi wa eneo hilo kuhama Mei 6.

Wapalestina waliolazimika kuyahama makazi yao kufuatia mashambulizi ya anga na ardhini ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza wanawasili kwenye kambi ya magharibi mwa Rafah, Gaza, Ijumaa, Mei 10, 2024.
Wapalestina waliolazimika kuyahama makazi yao kufuatia mashambulizi ya anga na ardhini ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza wanawasili kwenye kambi ya magharibi mwa Rafah, Gaza, Ijumaa, Mei 10, 2024. AP - Abdel Kareem Hana
Matangazo ya kibiashara

"Hadi sasa, karibu wakazi 300,000 wamehamia eneo la  la Al-Mawassi", kilomita chache kutoka Rafah, jeshi limebaini katika taarifa. 

Jeshi linaandaa mashambulizi ya ardhini katika mji huu ambapo baadhi ya wakazi milioni 1, 4, wengi walisukumwa pale na mapigano, wakiwa wamekusanyika pamoja.

Wakati huo huo Israeli imetangaza amri nyengine mpya kwa raia wa Gaza kuondoka  kusini mwa mji wa Rafah wakati huu inapojiandaa kupanua oparesheni zake za kijeshi katika eneo hilo.

Kando na agizo hilo, Israeli pia imesema inaelekea kaskazini mwa Gaza ambako inasema wapiganaji wa Hamas wamekusanyika tena.

Mapigano yameripotiwa kuongezeka katika Ukanda wa Gaza ambako makabiliano mazito kati ya Hamas na wanajeshi wa Israeli yameendelea kuripotiwa viungani mwa mji wa Rafah.

Tayari raia wa Palestina zaidi ya laki moja wamethibitishwa kutorokea katika maeneo ya kaskazini wakihofia kushambuliwa na wanajeshi wa Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.