Pata taarifa kuu

Gaza: Israeli imetoa amri nyengine kwa wakaazi wa Rafah kuondoka

Israeli imetangaza amri nyengine mpya kwa raia wa Gaza kuondoka  kusini mwa mji wa Rafah wakati huu inapojiandaa kupanua oparesheni zake za kijeshi katika eneo hilo.

Kando na agizo hilo, Israeli pia imesema inaelekea kaskazini mwa Gaza ambako inasema wapiganaji wa Hamas wamekusanyika tena.
Kando na agizo hilo, Israeli pia imesema inaelekea kaskazini mwa Gaza ambako inasema wapiganaji wa Hamas wamekusanyika tena. REUTERS - Hatem Khaled
Matangazo ya kibiashara

Kando na agizo hilo, Israeli pia imesema inaelekea kaskazini mwa Gaza ambako inasema wapiganaji wa Hamas wamekusanyika tena.

Mapigano yameripotiwa kuongezeka katika Ukanda wa Gaza ambako makabiliano mazito kati ya Hamas na wanajeshi wa Israeli yameendelea kuripotiwa viungani mwa mji wa Rafah.

Tayari raia wa Palestina zaidi ya laki moja wamethibitishwa kutorokea katika maeneo ya kaskazini wakihofia kushambuliwa na wanajeshi wa Israeli.

Soma piaRaia wa Palestina zaidi ya laki moja wametoroka katika mji wa Rafah

Washirika wa Israeli ikiwemo nchi ya Marekani wameionya dhidi ya kutekeleza oparesheni hiyo katika mji wa Rafah wenye idadi kubwa ya raia waliotoroka mapigano kutoka katika maeneo mengine.

Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa nayo yanasema kwamba yanapata ugumu wa kuwasilisha misaada katika eneo la Gaza baada ya wanajeshi wa Israeli kufunga baadhi ya maeneo muhimu, Israeli kwa upande wake ikisema imefungua baadhi ya maeneo ya mipaka.

Umoja wa Mataifa kwa upande wake umeendelea kusisitiza kwamba iwapo Israeli itatekeleza oparesheni hiyo basi huenda ikawa ni pigo kubwa kwa mchakato wa utoaji wa misaada ya kibinadamu.

Soma piaGuterres: Mashambulizi ya ardhini ya Israel huko Rafah yatasababisha 'janga kubwa la kibinadamu'

Kwa sasa zaidi ya raia wa Palestina milioni moja, nusu ya idadi ya raia wa Gaza, wamekuwa wakipata hifadhi katika mji wa Rafah.

Jumatatu ya wiki hii, jeshi la Israeli lilitoa amri yake ya kwanza kwa raia wa mashariki mwa Rafah kuondoka likisema lilikuwa katika maandalizi ya shambulio la ardhini kuwasaka Hamas.

Israeli imeendelea kutekeleza mashambulio katika ukanda wa Gaza baada ya mazungumzo kukwama mjini Cairo.
Israeli imeendelea kutekeleza mashambulio katika ukanda wa Gaza baada ya mazungumzo kukwama mjini Cairo. REUTERS - Hatem Khaled

Aidha jeshi la Israel limethibitisha kuwa takriban raia 300,000 wa Gaza wamehama kutoka kwenye eneo wanapotarajiwa kutekeleza oparesheni za kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.