Pata taarifa kuu

Israel: Netanyahu aahidi kuingia Rafah 'kwa makubaliano au la'

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameahidi siku ya Jumanne kwamba jeshi la Israel litaingia Rafah, mji ulioko kusini mwa Ukanda wa Gaza, iwapo makubaliano ya kusitisha mapigano yanayotarajiwa yatahitimishwa na kundi la Hamas. 

Premieru israelian, Benjamin Netanyahu și liderul Hamas în Gaza, Yahya Sinwar
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu (kushoto) na kiongozi wa Hamas huko Gaza, Yahya Sinwar. © Associated Press
Matangazo ya kibiashara

"Wazo kwamba tutasimamisha vita kabla ya kufikia malengo yetu yote ni ndoto na hayaendani na wsali hili. Tutaingia Rafah na kukomesha vita vya Hamas, kwa makubaliano (ya usitishwaji vita) au la, ili kupata ushindi kamili," Netanyahu alinukuliwa akisema katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake kwa wawakilishi wa familia zilizotekwa huko Jerusalem.

Hayo yanajiri wakati wajumbe wa makundi ya wapiganaji wa Kipalestina ya Hamas na Fatah wamekutana kwa mazungumzo mjini Beijing na kutangaza nia yao ya kufikia maridhiano.

Makundi hasimu ya wapiganaji wa Kipalestina ya Hamas na Fatah wameeleza nia yao ya kisiasa ya kutaka  maridhiano kwa njia ya mazungumzo walipokutana mjini Beijing. Hayo yameelezwa hii leo na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Lin Jian.

Maafisa wa kundi la Hamas wameondoka mjini Cairo baada ya mazungumzo na maafisa wa upatanishi wa Misri kuhusu pendekezo jipya la kusitisha mapigano huko Gaza. Kituo cha Televisheni cha Al-Qahira News, ambacho kina mafunganamo na idara ya ujasusi ya Misri, kimesema ujumbe wa Hamas utarejea mjini Cairo na jibu rasmi la maandishi kuhusu pendekezo hilo, bila hata hivyo kuelezea wazi siku hiyo

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.