Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Gaza: Baada ya Afrika Kusini kuwasilisha malalamiko yake, Israel yajitetea mbele ya ICJ

Mnamo Januari 26, Mahakama ya Kimataifa ya Haki iliamua kwamba kulikuwa na "hatari" ya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina huko Gaza, kufuatia malalamiko kutoka Afrika Kusini kushutumu taifa la Kiyahudi kwa kukiuka Mkataba wa Mauaji ya Kimbari. Mwanzoni mwa mwezi wa Machi, Pretoria iliwataka majaji kumi na watano kuagiza Israeli kuondoa vikwazo, kutangaza vikwazo vya silaha na kuagiza kumalizika kwa mzozo huo. Majibu ya Israel kwa Afrika Kusini.

Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) wakitoa uamuzi wao kuhusu Israel, huko Hague, Uholanzi, Januari 26, 2024 (picha ya kielelezo).
Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) wakitoa uamuzi wao kuhusu Israel, huko Hague, Uholanzi, Januari 26, 2024 (picha ya kielelezo). © PIROSCHKA VAN DE WOUW / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Hague, Stéphanie Maupas

Majibu ya Israeli ni ya kutisha. Serikali ya Israel inaishutumu Afrika Kusini kwa kufanya utaratibu huu "kujifurahisha", kwa kutumia vibaya Mahakama ya Dunia, na "kupotosha" ukweli.

Haishangazi, kwa hivyo Israeli inakataa hatua zote mpya zilizoombwa na Afrika Kusini. Katika kurasa 21, taifa la Israel linadai kuwa "linafanya mengi" kupunguza mateso ya raia huko Gaza, wakati watu wasiopungua 32,000 wameuawa katika eneo hilo tangu Oktoba 8.

Israel inakanusha kutaka kuwaua kwa njaa raia huko Gaza. Na katika aya kadhaa, wanasheria wake wanataja misaada ya kibinadamu inayotolewa kwa njia ya barabara, anga, na sasa baharini. Majibu ya Israel yanatoa hisia kwamba hali imedhibitiwa, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akizungumzia ukosefu wa usalama usio na kifani katika kiwango chake, kwani unaathiri zaidi ya watu milioni moja wa Gaza.

Katika ombi lake, Afrika Kusini inawataka majaji kuagiza mataifa yote kutekeleza Mkataba wa Mauaji ya Kimbari - huusan vikwazo vya silaha. Lakini Israeli inakumbusha kwamba mataifa mengine hayashiriki katika kesi hii na kwamba majaji hawawezi kuwaagiza chochote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.