Pata taarifa kuu

Israel: Hisia kali baada ya kiongozi wa maseneta wa chama cha Democratic kumshtumu Netanyahu

Ni kiongozi wa chama cha Democratic katika Bunge la Seneti, pengine mwanasiasa mashuhuri wa Kiyahudi nchini Marekani. Amekuwa mfuasi asiyeyumba wa Israeli kwa miongo kadhaa. Chuck Schumer anamshambulia kwa ukali Benjamin Netanyahu ambaye, anasema, anafuata masilahi yake binafsi na hatari ya kuibadilisha Israeli kuwa gumzo katika jamii ya kimataifa. Na anatoa wito kwa Israeli kuandaa uchaguzi mpya haraka iwezekanavyo. Maneno ambayo yamepokelewa vibaya na viongozi wa Israel.

Kiongozi wa wengi wa chama cha Democratic katika Bunge la Seneti la Marekani, Chuck Schumer, mjini Washington, Desemba 5, 2023.
Kiongozi wa wengi wa chama cha Democratic katika Bunge la Seneti la Marekani, Chuck Schumer, mjini Washington, Desemba 5, 2023. REUTERS - KEN CEDENO
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul

Hisia mbalimbli zimetolewa baada ya kiongozi wa chama cha Democratic katika Bunge la Seneti, Chuck Schumer, kumshtumu Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Likud, chama cha Israel cha Benjamin Netanyahu kinasema ni demokrasia huru na ya kujivunia ambayo ilimchagua Waziri Mkuu wake, na sio jamhuri ya majambazi. Walio karibu na Netanyahu pia wanasisitiza kuwa sera anayofuata inaungwa mkono na idadi kubwa ya watu.

Kwa upande mwingine, Benny Gantz, mjumbe wa baraza la mawaziri la vita, lakini pia mpinzani mkuu wa kisiasa wa Benjamin Netanyahu, anabaini kwamba rafiki mkubwa wa Israel Chuck Schumer wakati huu amefanya makosa kwa kuingilia masuala ya ndani ya nchi. Yair Lapid, kiongozi wa upinzani wa Israel, anabainisha kuwa Netanyahu anapoteza wafuasi muhimu wa Israel nchini Marekani mmoja baada ya mwingine. Mbaya zaidi, anafanya kwa makusudi, ameongeza mwanasiasa huyo wa upinzani wa Israel.

Uhusiano kati ya Israel na Marekani umefikia kiwango cha mvutano, wahariri kadhaa wanatangaza. Maoni ya Chuck Schumer yanaumiza sana, inasemekana hapa, kwa sababu yuko, na ataendelea kuwa, mmoja wa wafuasi wenye shauku wa Israeli katika Bunge la Marekani. Na kwamba wanafuata ukosoaji mkali kutoka kwa Joe Biden na Makamu wa Rais wa Marekani. Na Ijumaa hii asubuhi, Gazeti la kila siku la mrengo wa kushoto la Haaretz linadai kwamba Schumer amefanya kile alichopaswa kufanya: kulinda Israeli dhidi yake.

Ama kuhusu Netanyahu, bado amedhamiria zaidi kuliko hapo awali kuendelea na sera yake na haswa kutekeleza mashambulizi huko Rafah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.