Pata taarifa kuu

Gaza: Mkuu wa diplomasia ya Ulaya alaani 'mauaji mapya' na 'vifo visivyokubalika kabisa'

Mkuu wa diplomasia ya Ulaya Josep Borrell ameshutumu siku ya Alhamisi usiku "mauaji mapya" na vifo "visivyokubalika kabisa" baada ya vifo vilivyotangazwa na Hamas vya zaidi ya watu 110 wakati wa usambazaji wa misaada huko Gaza, zoezi ambalo liligeuka kuwa machafuko.

Watu waliojeruhiwa katika hospitali ya Kamal Edwan huko Beit Lahia baada ya jeshi la Israel kuwafyatulia risasi raia waliokuwa wakikimbilia kwenye malori ya misaada ya kibinadamu, Februari 29, 2024.
Watu waliojeruhiwa katika hospitali ya Kamal Edwan huko Beit Lahia baada ya jeshi la Israel kuwafyatulia risasi raia waliokuwa wakikimbilia kwenye malori ya misaada ya kibinadamu, Februari 29, 2024. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

"Nimeshtushwa na ripoti za mauaji zaidi kati ya raia huko Gaza ambao walikuwa wakitamani kupata msaada wa kibinadamu," Josep Borrell amesema kwenye mtandao wa kijamii wa X. "Vifo hivi havikubaliki kabisa."

Wizara ya Afya ya Hamas iliripoti takriban watu 104 waliofariki na 760 kujeruhiwa katika mji wa Gaza wakati wa usambazaji wa misaada ya kibinadamu, zoezi ambalo liligeuka kuwa machafuko, ikilaani "mauaji" hayo. Vyanzo vya Israeli vinathibitisha risasi za moto.

Zaidi ya raia mia moja wamefariki na takriban 760 wamejeruhiwa wakati walipoingia kwenye malori ya misaada ya kibinadamu kaskazini mwa Ukanda wa Gaza walipokuwa wakisubiri lori za misaada ya kibinadamu mnamo Alhamisi Februari 29, kulingana na Wizara ya Afya ya Hamas, iliyoko madarakani katika Ukanda wa Gaza. Msemaji wa wizara ya afya ya Hamas Ashraf al-Qudra alisema katika taarifa yake kwamba, idadi ya watu waliofariki kutokana na mauaji katika Mtaa wa al-Rashid katika mji wa Gaza imefikia 104 na wengine 760 kujeruhiwa. Ripoti ya awali ya hospitali ilisema vifo vya watu 50

Ili kueleza kilichotokea, mkurugenzi wa dharura wa hospitali ya al-Chifa katika mji wa Gaza, Amjad Aliwa, pamoja na mashahidi kadhaa liliambia shirika la habari la AFP kwamba wanajeshi wa Israel waliwafyatulia risasi "maelfu ya raia" waliokuwa wakikimbilia lori za misaada ya kibinadamu kwenye randabauti ya upande wa magharibi wa mji, wakati wakaazi wa eneo hilo walikuwa wakikabiliwa na njaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.