Pata taarifa kuu

Washington haikubakubaliani na tangazo upanuzi wa makazi katika Ukingo wa Magharibi

Israel imetangaza ujenzi wa maelfu ya nyumba katika makazi ya Ukingo wa Magharibi, mara baada ya tukio la ufyatuaji risasi siku ya Alhamisi, Februari 22, ambalo lilisababisha kifo cha raia mmoja wa Israeli. Watu wengine 11 walijeruhiwa katika shambulio hilo, huku wahusika watatu wakiuawa. Uamuzi huo wa Israel unadhoofisha uhusiano na Marekani ambao unaendelea kuzorota.

Mwonekano wa makazi ya Waisraeli yaliyoanzishwa katika Ukingo wa Magharibi huko Maale Adumim, hapa ilikuwa tarehe 18 Juni 2023.
Mwonekano wa makazi ya Waisraeli yaliyoanzishwa katika Ukingo wa Magharibi huko Maale Adumim, hapa ilikuwa tarehe 18 Juni 2023. AP - Mahmoud Illean
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul

Kwa mujibu wa Betsalel Smotrich, waziri wa Israel mwenye msimamo mkali zaidi, idhini kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 3,000 katika makazi ya Ukingo wa Magharibi ini jibu mwafaka la Wazayuni. Sehemu kubwa ya makao haya yataanzishwa huko Maale Adumim, hasa ambapo tukiola ufyatuaji risasi ulifanyika asubuhi ya Alhamisi Februari 22. Maeneo matatu ya kuanza tena kwa ujenzi huu, kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita, yako upande wa magharibi wa kizuizi cha usalama, katika maeneo ambayo yanachukuliwa kuwa ya makubaliano zaidi.

Lakini majibu ya Marekani hayakuchukua muda mrefu kuanguka. Na yamekuwa ya kuchukiza: Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ametangaza kusikitishwa na tangazo la Israeli. "Makazi katika Ukingo wa Magharibi hayakubaliani na sheria za kimataifa," amesisitiza Antony Blinken. Haya ni mabadiliko ya ghafla ya sera na utawala wa Marekani: Mafundisho ya Pompeo - yaliyopewa jina la Mike Pompeo, mtangulizi wa Blinken - yamefutiliwa mbali. Mkuu wa zamani wa diplomasia ya Marekani, chini ya Donald Trump, alieleza kuwa makazi ya Waisraeli yenyewe hayapingani na sheria za kimataifa.

Hii ikiwa ni hatua mpya ya makabiliano kati ya Israel na Marekani, na kuonyesha nguvu kutoka kwa Israel ya mrengo wa kulia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.