Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa washutumu 'tabia mbaya ya kimaadili' ya Israeli baada ya shutuma dhidi yake

Ripota wa Umoja wa Mataifa Francesca Albanese amesema kuhusu hali ya haki za binadamu katika maeneo ya Palestina kwamba "mashambulizi yasiyo na msingi ya Israel dhidi ya Umoja wa Mataifa yanaonyesha tu tabia mbaya ya kimaadili."

Francesca Albanese, ripota maalum kuhusu hali ya haki za binadamu katika ardhi maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu.
Francesca Albanese, ripota maalum kuhusu hali ya haki za binadamu katika ardhi maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu. AP - Salvatore Di Nolfi
Matangazo ya kibiashara

Mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa ameongeza katika taarifa yake, baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel kutangaza kutoongeza muda wa visa vya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwamba "Umoja wa Mataifa umedhoofishwa na miongo kadhaa ya kutoadhibu kwa ukiukaji wa sheria za kimataifa, ikiwa ni pamoja na ukoloni wa maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na wWapalestina kulazimishwa kuhama makazi yao. ”

Pia amesema kwamba “Umoja wa Mataifa lazima uwajibishe Israeli ikiwa unataka kuokoa sifa na madhumuni yake,” akisisitiza kwamba “hakuna anayeweza kuwa huru ikiwa kila mtu hayuko huru.” Mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano, kuachiliwa kwa mateka na wafungwa wa Kipalestina, ulinzi kamili, ujenzi mpya, kukomesha ukaliaji na haki.

Ripoti mpya kutoka kwa Wizara ya Afya ya Hamas ambayo inataja vifo vya Wapalestina 21,110

Wizara ya Afya ya Palestina inayoongozwa na Hamas ilmetangaza siku ya Jumatano kwamba operesheni za kijeshi za Israel katika Ukanda wa Gaza zimesababisha vifo vya watu 21,110 tangu vita hivyo vilipoanza Oktoba 7. Idadi hii inajumuisha watu 195 waliouawa katika saa 24 zilizopita, imesema wizara hiyo, ambayo pia imeripoti majeruhi 55,243 tangu tarehe hiyo.

UNRWA yaonya kuhusu hali ya afya kusini mwa Ukanda wa Gaza

Juliette Touma, mkurugenzi wa mawasiliano wa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina, anazungumzia hali ya afya inayowakabili Wapalestina na anazungumzia "choo kimoja cha watu 400", "zaidi ya watu 100,000 waathirika wa ugonjwa wa kuhara" au watu wengi wenye matatizo ya kupumua. Magonjwa ambayo huenea kwa haraka zaidi katika hali ndogo au hata zisizo za usafi.

 Rais Erdoğan wa Uturuki amlinganisha Benjamin Netanyahu na Adolf Hitler

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, katika hafla ya utoaji tuzo mjini Ankara, Erdoğan alimlinganisha Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Adolf Hitler na mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza kwa mateso ya Wanazi waliotendea Wayahudi. "Watatufanya tukumuke mengi aliyoyafanya Hitler. Je, kuna tofauti katika matendo ya Netanyahu ikilinganishwa na ya Hitler? ", amesema. Erdoğan ameongza kuwa Marekani ilihusika katika vifo vya watu 20,000 huko Gaza kwa sababu "iliunga mkono" Israeli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.