Pata taarifa kuu

Israel yapanua operesheni zake Gaza wakati hali ya wasiwasi ikiongezeka

Jeshi la Israel linapanua operesheni zake katika Ukanda wa Gaza siku ya Jumatatu, ambapo idadi ya vifo miongoni mwa raia wa Palestina inaongezeka, huku dalili mpya za mzozo zikienea katika eneo hilo na matukio ya wikendi hii nchini Iraq na katika Bahari Nyekundu.

Katika Hospitali ya Deir al Balah Jumapili Desemba 3, 2023.
Katika Hospitali ya Deir al Balah Jumapili Desemba 3, 2023. AP - Hatem Moussa
Matangazo ya kibiashara

"Jeshi la Israel linaendelea kupanua operesheni yake ya ardhini dhidi ya Hamas katika eneo lote la Ukanda wa Gaza. Jeshi linafanya kazi popote pale ambapo Hamas ina ngome," msemaji wake, Daniel Hagari, alisema Jumapili jioni.

Wanajeshi wa Israel wamekuwa wakifanya mashambulizi ya ardhini tangu Oktoba 27 kaskazini mwa Gaza, ambapo wamedhibiti maeneo kadhaa. Tangu mapigano yaanze tena Ijumaa kufuatia kumalizika kwa usitishwaji wa mapigano wa wiki moja na Hamas, jeshi limekuwa likijikita zaidi kwa mashambulizi ya anga.

Mashambulizi ya anga usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu kwenye lango la hospitali ya Kamal Adwan, iliyoko kaskazini mwa Gaza, yalisababisha vifo vya watu kadhaa kwa mujibu wa shirika la Palestina la Wafa, huku serikali ya Hamas ikilishutumu jeshi la Israel katika taarifa kwa "ukiukaji mkubwa" wa sheria ya kimataifa ya ubinadamu.

Israel inaishutumu Hamas kwa kuweka miundombinu ndani au chini ya hospitali na kutumia raia kama ngao za binadamu.

Wizara ya Afya ya Hamas ilisema Jumapili kwamba watu 15,523, 70% yao wakiwa wanawake na watoto, wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza, yaliyotekelezwa kujibu shambulio la umwagaji damu la Oktoba 7 la kundi la Hamas dhidi ya Israeli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.