Pata taarifa kuu

Hamas yadai kutekeleza shambulio baya Jerusalem na kutoa wito 'mapigano zaidi'

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas kutoka Palestina Hamas limedai kuhusika na shambulio la risasi lililosababisha vifo vya watu watatu mjini Jerusalem siku ya Alhamisi na kutoa wito wa "mapigano ya ukombozi" dhidi ya Israel.

Polisi na maafisa wa idara ya huduma za dharura katika eneo la shambulio huko Jerusalem, Novemba 30, 2023.
Polisi na maafisa wa idara ya huduma za dharura katika eneo la shambulio huko Jerusalem, Novemba 30, 2023. AP - Ohad Zwigenberg
Matangazo ya kibiashara

"Ndugu Mourad Nemr (umri wa miaka 38) na Ibrahim Nemr (umri wa miaka 30) [...], wanachama wa brigedi ya Ezzedine al-Qassam ya Sour Baher", wilaya ya Jerusalem Mashariki "wamejitoa mhanga kwa kufanya operesheni ” ambayo "imeua walowezi watatu na kuwajeruhi wengine," Hamas imesema katika taarifa. Polisi wa Israel wamethibitisha kuwa washambuliaji hao wawili, ndugu kutoka Jerusalem Mashariki, waliuawa kwa kupigwa risasi.

Polisi na maafisa wa idara ya huduma za dharura katika eneo la shambulio huko Jerusalem, Novemba 30, 2023.
Polisi na maafisa wa idara ya huduma za dharura katika eneo la shambulio huko Jerusalem, Novemba 30, 2023. AP - Ohad Zwigenberg

Wakati huo huo wanajeshi wawili wa Israel wamejeruhiwa kidogo katika shambulio la gari kwenye kituo cha ukaguzi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu siku ya Alhamisi, jeshi la Israel limesema, na kuongeza kuwa mshambuliaji "ameangamizwa." Jeshi "linafanya msako katika eneo hilo kuwatafuta washukiwa wengine," limeongeza katika taarifa. Shambulio hilo linakuja baada ya kuongezwa kwa siku moja kwa muda wa usitishwaji wa mapigano kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Mpalestina auawa katika Ukingo wa Magharibi

Mapigano yalizuka kabla ya mapambazuko kati ya Wapalestina na wanajeshi wa Israel nje ya jela ya Israel ya Ofer karibu na Ramallah katika Ukingo wa Magharibi. Raia mmoja wa Palestina aliuawa kwa risasi na jeshi la Israel, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina. Shirika la habari la Palestina WAFA lilimtambua mwathiriwa huyo kuwa ni kijana wa miaka 21 kutoka kijiji kimoja magharibi mwa Ramallah.

Tangu Oktoba 7, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, karibu Wapalestina 250 wameuawa na wanajeshi wa Israel au walowezi katika Ukingo wa Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.