Pata taarifa kuu

Israel yawaita mabalozi wa Ubelgiji na Uhispania

Israel imeamua kuwaita mabalozi wa Ubelgiji na Uhispania kwa "karipio kali" baada ya wakuu wa serikali kushutumu kutoka Misri "maangamizi ya Gaza" na kuitaka Israeli "kulitambua taifa la Palestina". Mkuu wa diplomasia ya Israel, Eli Cohen, "ameagiza kuwaita mabalozi wa nchi hizi kwa mazungumzo ya karipio kali," ofisi yake ilmetangaza. Kulingana waziri wa mambo ya nje wa Israel, viongozi hao wawili "wanaunga mkono ugaidi".

Mkuu wa diplomasia ya Israel, Eli Cohen.
Mkuu wa diplomasia ya Israel, Eli Cohen. AP - Burhan Ozbilici
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa tofauti, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu "amelaani vikali" maoni yao, akiwashutumu kwa kushindwa "kuhusisha uwajibikaji kamili kwa Hamas kwa uhalifu dhidi ya binadamu iliofanya kwa kuua raia wetu na kutumia Wapalestina kama ngao za kibinadamu.

Akitembelea kituo cha Rafah cha Misri siku ya Ijumaa, Waziri Mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo alibaini kwamba jibu la Israel katika Ukanda wa Gaza baada ya shambulio baya la Hamas nchini Israel mnamo Oktoba 7 lazima "liheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu". "Vifo vya raia lazima vikome," alisisitiza waziri wa Ubelgiji.

Kando yake, mwenzake wa Uhispania Pedro Sanchez, ambaye alikutana naye na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi siku ya Ijumaa mjini Cairo, aliitolea wito "Israel kuwa ya kwanza kuwa na mtazamo mpana ikiwa ni pamoja na Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki", akitoa wito kwa " kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa na Israel ya taifa la Palestina”.

Mkuu wa diplomasia ya Uhispania, José Manuel Albares, alielezea "mashtaka ya serikali ya Israeli" dhidi ya kiongozi wa Uhispania na Ubelgiji kuwa "ya uwongo, hayana umuhimu na hayakubaliki", katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.