Pata taarifa kuu

UNRWA yatangaza shambulio la pili lililolenga shule inayotumika kama kimbilio kaskazini mwa Gaza

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, limetangaza hivi punde kwamba shule ya pili imekuwa ikilengwa na mashambulizi kaskazini mwa Gaza. Jengo hilo linatumika kama kimbilio salama ya watu zaidi ya 4,000 kufuatia mashambulio ya Israel.

Moshi mwingi juu ya Jiji la Gaza, Ijumaa Novemba 17, 2023.
Moshi mwingi juu ya Jiji la Gaza, Ijumaa Novemba 17, 2023. AP - Leo Correa
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kufahamu:

► UNRWA inatangaza shambulio jipya la anga kwenye moja ya shule zake kaskazini mwa Gaza ambalo limekuwa likitoa hifadhi kwa zaidi ya watu 4,000. Shirika la Umoja wa Mataifa linahakikisha kwamba "makumi ya watu waliuawa, ikiwa ni pamoja na watoto".

► Siku ya Jumamosi Hamas ilitangaza kuwa Wapalestina 12,300 wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita Oktoba 7. Kati yao, zaidi ya watoto 5,000 na wanawake 3,300.

► Mamia ya watu walihamishwa Jumamosi, Novemba 18, kutoka hospitali ya Al-Shifa, kubwa zaidi huko Gaza, ambako, kulingana na Umoja wa Mataifa, kulikuwa na wagonjwa wasiopungua 2,300, madaktari na watu waliokimbia makazi yao waliokwama kutokana na vita. Wahudumu wa afya wamesema wagonjwa 120, wakiwemo watoto wanaozaliwa kabla ya wakati, bado wako kwenye kituo hicho.

► Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linaonya kuhusu "hatari ya haraka ya njaa" katika Ukanda wa Gaza. "Hatuulizi mwezi. Tunatoa wito wa kuchukuliwa hatua za kimsingi zinazohitajika ili kukidhi mahitaji muhimu ya raia na kukomesha hali ya janga hili,” amesema mkuu wa operesheni za kibinadamu za Umoja wa Mataifa, Martin Griffiths.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.