Gaza: Israeli yadaiwa kuamuru kuondolewa kwa watu katika hosipitali ya Al-Shifa
Nairobi – Wanajeshi wa Israeli wamedaiwa kutaka watu walio katika hosipitali ya Al-Shifa kuondolewa kwa haraka, tangazo linalokuja wakati huu maofisa hao wa Israeli wakiendelea na oparasheni katika hosipitali hiyo kwa madai kuwa wapiganaji wa Hamas wanajificha humo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Al-Shifa, ni hosipitali kubwa zaidi katika ukanda wa Gaza na imekuwa kitovu cha mapigano kati ya Israeli na wapiganaji wa Hamas wiki hii.
Agizo hilo linalodaiwa kutoka kwa jeshi la Israeli linakuja wakati huu makabiliano kati yake na wapiganaji wa Palestina, Hamas yakiingia wiki ya saba tangu Hamas kutekeleza shambulio tarehe 7 ya mwezi Oktoba Kusini mwa Israeli.
Israel imekuwa ikidadi kuwa wapiganaji wa Hamas wanatumia hosipitali ya Al-Shifa, kama kituo chao cha kamandi madai ya ambao Hamas imekanusha.
Umoja wa Mataifa umekadiria kuwa karibia wagonjwa 2,300, wahudumu wa hosipitali hiyo na raia wengine wa Palestina ambao walikuwa wanapewa hifadhi katika kituo hicho kabla ya uvamizi wa Israeli siku ya Jumatano.
Wizara ya afya katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa idadi kubwa ya wagonjwa waliofariki katika kituo hicho ilisababishwa na kukatwa kwa umeme, ukosefu wa mafuta uliosababishwa na mapigano mazito yanyoendelea.
Israel imekuwa ikisisitiza wagonjwa kuhamishiwa kusini mwa eneo hilo lakini wahudumu wa afya kwenye hosipitali hiyo wanasema kuwa wagonjwa hao hawawezi kuondolewa katika hali ya sasa.
Kwa mujibu wa mkurungenzi mkuu katika hoispitali hiyo Mohammed Abu Salmiya amesema wanajeshi wa Israeli wamemtaka kuwaondoa wagonjwa, watu waliojeruhiwa na waliomba hifadhi pamoja na wahudumu wa afya na kuwapeleka katika eneo la kusini kwa miguu bila ya kutumia magari ya wagonjwa.