Pata taarifa kuu

Washington yapinga 'kukaliwa upya' kwa Gaza na Israel

Wakati Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu akitangaza siku ya Jumatatu, Novemba 6, kwamba anataka kuchukua "jukumu la jumla kwa usalama" wa Gaza baada ya vita, Washington imetoa msimamo wake siku ya  Jumanne, ikisema kuwa inapinga ukaliaji wa muda mrefu wa eneo hilo na Israeli.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwa na wanajeshi wake kutoka kambi ya kijeshi ya Tze'elim, Novemba 7, 2023.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwa na wanajeshi wake kutoka kambi ya kijeshi ya Tze'elim, Novemba 7, 2023. via REUTERS - GPO/HAIM ZACH
Matangazo ya kibiashara

"Kwa maoni yetu, Wapalestina lazima wawe katikati ya maamuzi haya, Gaza ni eneo la Palestina na itabaki kuwa eneo la Palestina," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Vedant Patel amewaambia waandishi wa habari.

"Kwa ujumla, hatuungi mkono kukaliwa tena kwa Gaza na Israel pia haiungi mkono," ameongeza.

Israel iliwaondoa kwa upande mmoja wanajeshi wake na walowezi kutoka Gaza mwaka 2005 baada ya kukalia eneo hilo kwa miaka 38. Israel imeweka kizuizi cha kuingia na kutoka Gaza tangu mwaka 2007, wakati kundi la wanamgambo wa Hamas liliposhinda uchaguzi na kupata mamlaka ya kuongoza Palestina.

"Haiwezekani kurudi kwenye hali ilivyo"

Washington inatambua "kwamba haiwezekani kurejea katika hali iliyokuwepo" kabla ya shambulio la umwagaji damu la Oktoba 7.

"Israel na ukanda mzima lazima viwe salama na Gaza haipaswi na haiwezi tena kuwa kituo ambacho mashambulizi ya kigaidi yanaanzishwa dhidi ya watu wa Israeli au mtu mwingine yeyote," ameongeza.

Benjamin Netanyahu alitangaza siku ya Jumatatu jioni kwamba nchi yake itachukua "kwa muda usiojulikana, jukumu la jumla la usalama" katika eneo la Palestina baada ya vita, kuzuia, kurudi kwa Hamas, amesema.

Wanajeshi wa Israel wamekuwa wakishambulia kwa mabomu Gaza na kuzidisha mashambulizi yao ya ardhini kujibu mashambulizi ya umwagaji damu ya tarehe 7 Oktoba. Zaidi ya Wapalestina 10,000 waliuawa na zaidi ya 20,000 kujeruhiwa kwa mujibu wa serikali ya Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.