Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin anazuru Israeli
Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, amewasili nchini Israeli katika ziara inayolenga kuonyesha mshikamano na taifa hilo baada ya kushambuliwa na wapiganaji wa Hamas ambalo limesababisha vifo vya maelfu ya raia wake.
Imechapishwa:
Austin anatarajiwa kukutana na viongozi wa Israeli akiwemo waziri mkuu Benjamin Netanyahu, waziri wa ulinzi Yoav Gallant.
Just landed in 🇮🇱 Tel Aviv. Today, I’ll meet w/ Prime Minister @netanyahu, Minister @YoavGallant & other senior leaders to demonstrate that America’s support for Israel’s security is ironclad & talk to them face-to-face about their defense needs. We stand w/ the people of Israel. pic.twitter.com/O4y68Pckkw
— Secretary of Defense Lloyd J. Austin III (@SecDef) October 13, 2023
Hii ni ziara yake tatu nchini Israeli tangu kuteuliwa katika wadhifa huo na inakuja baada ya ile ya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken katika eneo hilo.
Haya yanajiri wakati huu idadi ya waliouawa katika eneo la Gaza ikifikia 1,537 wakiwemo watoto kwa mujibu wa wizara ya afya ya Gaza.
Kwa mujibu wa wizara hiyo, watu 500 waliouawa walikuwa chini ya umri wa miaka 18.
Tayari Israeli imewataka raia zaidi ya milioni moja wanaoishi katika eneo la kaskazini mwa Gaza kuondoka katika muda wa saa 24 kabla ya mashambulio ya ardhini yaliopangwa kuaanza, wito ambao wapiganaji wa Hamas wameukataa.