Pata taarifa kuu

Takriban watu 70 wauawa Israel katika mashambulizi ya Hamas

Idara ya Huduma za dharura nchini Israel imebaini kwamba imehesabu takriban watu 70 waliofariki nchini humo tangu kuanza kwa mashambulizi ya Hamas, ambayo imerusha maelfu ya maroketi kuelekea Israel, huku wapiganaji wa kundi hilo wakipenya na kuingia kwenye ardhi ya Israeli. 

Afisa wa polisi wa Israel akielekea kwenye gari linalowaka, kufuatia kurushwa kwa roketi kutoka Ukanda wa Gaza, shambulio la  tawi lenye silaha la Hamas, huko Ashkelon, Israel, Oktoba 7, 2023.
Afisa wa polisi wa Israel akielekea kwenye gari linalowaka, kufuatia kurushwa kwa roketi kutoka Ukanda wa Gaza, shambulio la tawi lenye silaha la Hamas, huko Ashkelon, Israel, Oktoba 7, 2023. REUTERS - SINAN ABU MAYZER
Matangazo ya kibiashara

 

Msemaji wa jeshi la Israel amebainisha kwamba "wanajeshi wa Israel na raia" walitekwa nyara na wapiganaji wenye silaha wa Hamas siku ya Jumamosi katika ardhi ya Israel. "Siwezi kutoa takwimu zozote kuhusu hilo kwa sasa. Huu ni uhalifu wa kivita ambao Hamas imefanya na italipa gharama yake,” msemaji wa jeshi amewaambia waandishi wa habari.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema nchi yake iko kwenye kile ambacho amekitaja kama vita na kundi la wanamgambo wa Palestina Hamas baada ya misururu ya maroketi kurushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel mapema leo Jumamosi.

Jeshi la Israel kwa upande wake limethibitisha kuwa linapambana na wapiganaji wa Gaza walioingia katika himaya kwa njia ya ardhini, baada ya maroketi kurushwa kuelekea Israeli kutoka katika eneo la Palestina.

Maelfu ya askari wa akiba wanatarajiwa kupelekwa huko Gaza, pamoja na kaskazini mwa Israel, karibu na Lebanon na Syria, na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu.

Hayo ni baada ya Hamas kutangaza kuwa imeanzisha operesheni 'Al-Aqsa Flood' dhidi ya Israel.

Makumi ya roketi zimerushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel Jumamosi asubuhi, Oktoba 7, na kusitisha makubaliano ya kusitisha uhasama yaliyoheshimiwa kwa ujumla tangu kumalizika kwa vita vya siku tano mwezi Mei. Tawi la kijeshi la Hamas limetangaza kwamba limeanzisha operesheni iitwayo "Mafuriko ya Al-Aqsa" dhidi ya Israel.

Brazil, ambayo kwa sasa inashikilia wadhifa wa urais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN), imetangaza Jumamosi Oktoba 7 kwamba itaitisha "mkutano wa dharura wa baraza hilo" kushughulikia hali nchini Israel na Ukanda wa Gaza. 

"Serikali ya Brazil inalaani mfululizo wa mashambulizi ya risasi na mashambulizi yaliyofanywa leo nchini Israel kutoka Ukanda wa Gaza," Wizara ya Mambo ya Nje imesema katika taarifa yake, ikitoa wito wa "kujizuia" kwa pande husika ili kuepusha mgogoro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.