Pata taarifa kuu

Ulaya kusaidia wanawake wa Afghanistan wanaoteswa na Taliban

Katika pendekezo lake la hivi punde kwa nchi Ishirini na Saba wanachama wa Umoja wa Ulaya, Shirika la Umoja wa Ulaya kwa ajili ya hifadhi kwa wakimbizi linazingatia kwamba ukweli tu wa kuwa mwanamke wa Afghanistan unapaswa kufanya uwezekano wa kupata hadhi ya ukimbizi.

Wanawake wa Afghanistan waandamana kupinga marufuku ya wanawake kwenda vyuo vikuu mnamo Desemba 22 huko Kabul.
Wanawake wa Afghanistan waandamana kupinga marufuku ya wanawake kwenda vyuo vikuu mnamo Desemba 22 huko Kabul. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwezi Agosti 2021, wwanawake nchini Afganistan wamekuwa wakiishi kwa kujitenga, wakifukuzwa nje ya nafasi ya umma na mamlaka mpya nchini Afghanistan, ambayo inawanyima haki ya elimu, kuwazuia kufanya kazi na kutembea kwa uhuru. Shirika la Umoja wa Ulaya kwa ajili ya hifadhi kwa wakimbizi (AUEA) linaona kuwa haki za wanawake sasa zinavujwa kinaga ubaga. Taasisi hii, ambayo inaratibu ulinzi wa wahamiaji barani Ulaya, inabaini kuwa ubaguzi dhidi ya wanawake wa Afghanistan unafikia kizingiti cha kutosha kuhitimu kuwa mateso.

"Leo hii, kuwa mwanamke nchini Afghanistan kunamaanisha kukabiliwa na hatua za vikwazo zilizowekwa na Taliban, katika suala la uhuru wa kujieleza, kutembea, kupata kazi, kupata elimu au matunzo, anasisitiza msemaji wa AUEA Andrew McKinlay. Mateso haya lazima yawape nafasi ya kupata hadhi ya ukimbizi. "

Idara za Umoja wa Ulaya zimefikia hitimisho hili ambalo halijawahi kushuhudiwa katika dokezo lao la hivi punde la mwongozo, lililowekwa hadharani tarehe 25 Januari 2023, ambalo linaorodhesha wasifu mahususi unaolengwa na waasi wa Kiislamu. Wanawake wanachukua nafasi kuu, pamoja na watetezi wa haki za binadamu, maafisa wa serikali ya zamani na Waafghan ambao wameunga mkono kwa njia moja au nyingine uingiliaji wa kijeshi wa NATO nchini Afghanistan.

Mapinduzi madogo kwenye karatasi

Kwa karatasi, mwongozo huu uliotolewa na AUEA ni mapinduzi madogo. Shirika hili linapendekeza kwamba mwanamke yeyote wa Afghanistan ambaye atabisha hodi kwenye milango ya nchi za Umoja wa Ulaya atapewa hadhi ya ukimbizi moja kwa moja. Katika mazoezi, hii haitakuwa hivyo, kwa sababu utawala wa ulinzi wa kimataifa wa Ulaya hutegemea nguzo mbili zisizoonekana.

Kwa upande mmoja, ni mara zote nchi wanachama ndizo zinazoamua katika hatua ya mwisho. Je, tunapaswa, ndiyo au hapana, kumkubali mtu huyu kwenye ardhi  yetu? Kila nchi kati ya nchi Ishirini na Saba wanachama wa Umoja wa Ulaya inaamua kwa njia ya uhuru, na hata kama, katika siku zijazo, mji mkuu huu au ule wa Ulaya unakataa ombi la mwanamke wa Afghanistan, Ulaya haitasema chochote.

Kwa upande mwingine, ni mchakato wa mtu binafsi. Kila nchi ya Ulaya huendesha, kupitia kwa mamlaka yake ya kitaifa, mahojiano ya kina na wanaotafuta hifadhi, ambao wanapaswa kueleza kwa kinaa ukatili ambao umewakuta, na ni baada ya uchunguzi wa kibinafsi wa faili yao kwamba uamuzi huchukuliwa.

Hata hivyo, tangu mwaka jana, mapendekezo ya Shirika la Ulaya yana thamani ya kisheria. Chukua mfano wa mwanamke wa Afghanistan ambaye ombi lake la hifadhi limekataliwa na mamlaka ya Ufaransa na ambaye anakata rufaa katika mahakama: katika kesi hii, majaji wa Ufaransa wana wajibu wa kuangalia ikiwa Ufaransa imezingatia uchambuzi wa mamlaka ya Ulaya kuhusu suala la Afghanistan, ikishindikana, Paris lazima ihalalishe, bila kukabiliwa na vikwazo.

Matarajio ya msingi ya utaratibu huu ni kuoanisha mazoea ya Ulaya, ili wanaotafuta hifadhi watendewe kwa njia sawa kila mahali katika Ulaya, bila kujali nchi ambako taratibu zao zinaanzia. Na hata kama hatuwezi kusema juu ya hali ya kulazimisha, maoni ya AUEA yalitoa athari zake za kwanza: baada ya Sweden, Tume ya Wakimbizi ya Denmark ilitangaza kwamba itatoa, kwa kigezo pekee cha jinsia, kibali cha kuishi kwa Waafghan wote, wanawake wanaoiomba, lakini pia kuangalia upya faili zote za wanawake au wasichana waliokataliwa na Denmark tangu kuanguka kwa Kabul.

Kwa tofauti chache, ni sawa kwa upande wa Ufaransa, ambapo kiwango cha ulinzi kilichotolewa kwa wanawake wa Afghanistan na Ofpra, Ofisi ya Ufaransa ya Ulinzi wa Wakimbizi na Watu Wasio na Uraia, tayari imefikia zaidi ya 95%, anakumbusha mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Julien Boucher. “Tulikuwa makini sana na hali mahususi ya wanawake na kwa haraka sana, tulianzisha utaratibu wa ulinzi ambao ni pamoja na kuzingatia kwamba, kwa ujumla wanawake wana hofu pindi wanaporejea Afghanistan na hivyo kuwa chini ya hadhi ya ukimbizi, ameainisha . Huu umekuwa msimamo wetu tangu mwanzo, kwa hivyo miongozo hii inakuja, kwa kadiri tunavyohusika, ili kuimarisha mazoezi ya ulinzi ambayo tayari yamekuwa yetu tangu katikati ya mwaka 2021. "

Kitu kigumu zaidi kwa wanawake hawa ni kutoka nje ya Afghanistan. Ikiwa watafanikiwa, Ulaya inaonekana imedhamiria kuungana na kuwafungulia milango. Na kuna kazi, kwa sababu kulingana na takwimu za hivi punde zilizopo, karibu maombi 15,000 ya hifadhi yaliwasilishwa katika Umoja wa Ulaya na raia wa Afghanistan kwa kipindi cha mwezi mmoja tu wa Novemba 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.