Pata taarifa kuu
MAREKANI-MASHARIKI YA KATI -AMANI

Antony Blinken amekamilisha ziara yake mashariki ya kati

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, ametamatizisha ziara yake katika eneo la Mashariki ya Kati, baada ya kukutana Jumanne na kiongozi wa Palestina Mahmud Abbas, baada ya kuonana na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, na kujadiliana kuhusu wasiwasi wa kiusalama kati ya Wapelestina na Waisraeli. 

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na waziri mkuu wa  Israeli  Benjamin Netanyahu
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu © via REUTERS / POOL
Matangazo ya kibiashara

Blinken, amesisitiza suluhu ya kudumu kati ya Israel na Palestina, ni kuundwa kwa mataifa mawili jirani yanayojitegemea ya Israeli na Palestina. 

“Tumeendelea kuwa wazi na kuendelea na msimamo wetu, kuwa kila upande uendelee kuwa makini ili kutochochea moto na kuendelea kutafakari suluhu ya muda mrefu ni kuwa na mataifa mawili yanayojitegemea, kinyume na hali ilivyo sasa.” amesema Antony Blinken

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, amekuwa kwa ziara ya siku nne katika eneo la mashariki ya kati.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.