Pata taarifa kuu
ISRAELI- PALESTINA

Israeli inapanga kubomoa makaazi ya Mpalestina, aliyewapiga risasi watu saba

Israeli inapanga kubomoa makaazi ya Mpalestina, aliyewapiga risasi watu saba na kuwauwa karibu na Sinagogi wiki iliyopita, Mashariki mwa mji wa Jerusalem.

Israeli inapanga kubomoa makaazi ya Mpalestina, aliyewapiga risasi watu saba
Israeli inapanga kubomoa makaazi ya Mpalestina, aliyewapiga risasi watu saba AP - Ariel Schalit
Matangazo ya kibiashara

Uongozi wa Israeli unasema hatua hiyo ni njia mojawapo ya kukabiliana na utovu wa usalama, wakati huu hali ya usalama kati yake na Palestina ikiendelea kuwa mbaya.

Aidha, Israeli imesema itawapokonya vibali vya kuishi vilovyotolewa kwa Wapelestina katika êneo la Mashariki mwa mji wa Jerusalem.

Wakati Israeli ikijiandaa kwa hatua hiyo, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amefanya mazungmzo na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, na kutoa wito wa utulivu, ili kuzuia uwezekano wa machafuko zaidi kushuhudiwa.

Naye Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, anatarajiwa mjini Jerusalem, leo kujadili mbinu za kuzuia machafuko zaidi na Waziri Mkuu Netanyahu na baadaye rais wa Palestina Mahmud Abbas.

Mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov, ametoa wito kwa Palestina na Israeli kuwa makini na kuchukua uwajibikaji mkubwa ili kuzuia hali kuwa mbaya.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.