Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Iraq yatia saini ushirikiano wa kimkakati na Ufaransa

Akiwa ziarani kwa muda wa siku mbili nchini Ufaransa, Waziri Mkuu wa Iraq alikutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron jioni ya Alhamisi Januari 26 kwa chakula cha jioni. Katika taarifa ya pamoja, viongozi hao wawili wanadai kuwa wametia saini mkataba wa ushirikiano wa kimkakati, na kuweka mfumo wa ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Katika hafla ya ziara ya kwanza ya Mohammed Chia al-Soudani mjini Paris, Emmanuel Macron ameahidi kuendeleza msaada wa Ufaransa katika mapambano dhidi ya ugaidi (picha yetu).
Katika hafla ya ziara ya kwanza ya Mohammed Chia al-Soudani mjini Paris, Emmanuel Macron ameahidi kuendeleza msaada wa Ufaransa katika mapambano dhidi ya ugaidi (picha yetu). AFP - CHRISTOPHE ARCHAMBAULT
Matangazo ya kibiashara

Katika hafla ya ziara ya kwanza ya Mohammed Chia al-Soudani mjini Paris, Emmanuel Macron aliahidi kuendeleza msaada wa Ufaransa katika mapambano dhidi ya ugaidi. Waziri Mkuu wa Iraq alitarajia, kabla ya ziara hiyo, kuimarisha ushirikiano huu kupitia mafunzo ya vikosi vya Iraq na ununuzi wa silaha. Lakini hakuna tangazo lililotolewa kuhusu hilo.

Vita dhidi ya rushwa

Kwa upande mwingine, mkataba wa maelewano ulitiwa saini kati ya Shirika la Kupambana na Ufisadi la Ufaransa na Tume ya Uadilifu ya Shirikisho la Iraq ili kupambana na ufisadi. Janga la kweli, nchi hiyo imeorodheshwa miongoni mwa nchi za mwisho na shirika la Transparency International.

Kuhusu suala la nishati, Ufaransa imeahidi tena kusaidia kukarabati mtandao wa umeme wa Iraq na uunganishaji wa umeme na Jordan. Ikulu ya Élysée inahakikisha kwamba huduma za mikopo zinazoweza kurejeshwa zitaongezwa kwa makampuni ya Ufaransa nchini Iraq. Ikiwa ni pamoja na TotalEnergie, iliyojitolea tangu 2021 kwa kandarasi ya dola bilioni kumi kujenga mtambo wa nguvu wa photovoltaic. Ujenzi bado haujaanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.