Pata taarifa kuu

Iraq: Mashambulizi ya Tehran dhidi ya upinzani wa Wakurdi wa Iran yaua tisa

Takriban watu tisa wameuawa na wengine 30 kujeruhiwa siku ya Jumatano katika eneo la Kurdistan la Iraq katika mashambulizi ya Iran dhidi ya makundi yenye silaha ya upinzani wa Wakurdi wa Iran, ambao wanalaani ukandamizaji wa maandamano katika Jamhuri ya Kiislamu.

Imedaiwa na Tehran, mashambulizi haya ya mabomu yalisababisha jumla ya watu tisa kupoteza maisha na 32 kujeruhiwa, waathiriwa ambao wako katika hospitali ya Erbil, mji mkuu wa mkoa unaojitawal.
Imedaiwa na Tehran, mashambulizi haya ya mabomu yalisababisha jumla ya watu tisa kupoteza maisha na 32 kujeruhiwa, waathiriwa ambao wako katika hospitali ya Erbil, mji mkuu wa mkoa unaojitawal. AFP - SAFIN HAMED
Matangazo ya kibiashara

 

Serikali ya shirikisho ya Iraq na mamlaka ya kikanda ya Kurdistan inayojitawa, kaskazini mwa nchi, imelaani mashambulizi ya makombora na mashambulizi mengine yaliyotekelezwa kulingana na Baghdad na "ndege 20 zisizo kuwa na rubani zilizojaa vilipuzi". Mahambulizi ambayo yamelenga maeneo manne. Televisheni ya taifa ya Iran imedai kuwa "vikosi vya ardhini vya Walinzi wa Mapinduzi vimeyalenga makao makuu kadhaa ya magaidi wanaotaka kujitenga kaskazini mwa Iraq kwa makombora ya uhakika na ndege zisizo na rubani".

Mashambulizi haya yamesababisha vifo vya watu tisa na wengine 32 kujeruhiwa, ametangaza Waziri wa Afya wa Kurdistan, Saman al-Barzanji, kutoka katika hospitali ya Erbil, mji mkuu wa mkoa unaojitegemea wa Kurdistan. Chama cha Kidemokrasia cha Kurdistan nchini Iran (PDKI), moja ya makundi yaliyolengwa na mashambulizi ya mabomu katika eneo la Koysinjaq, mashariki mwa Erbil, kimeripoti vifo viwili katika safu zake. Kwenye Twitter, PDKI ilikashifu "mashambulizi ya woga", yaliyotekelezwa wakati utawala wa Irani "hauwezi (...) kunyamazisha upinzani wa kiraia" wa Wakurdi na Wairani.

Mashambulizi haya yanakuja katika hali ya wasiwasi nchini Iran, ambapo maandamano ya usiku yamekuwa yakifanyika kila siku nchini humo tangu kifo cha Mahsa Amini, mwanamke mwenye umri wa miaka 22 aliyefariki baada ya kukamatwa na kikosi cha polisi cha kuheshimisha maadili. Maafisa wakuu mjini Tehran pia wamehusisha mashambulizi haya ya mabomu na "machafuko" ambayo yanaikumba Iran.

Kurdistan ya Iraq inakaribisha makundi kadhaa ya upinzani ya Kikurdi ya Irani ambayo kihistoria yamefanya uasi wa kutumia silaha dhidi ya Tehran, ingawa katika miaka ya hivi karibuni shughuli zao za kijeshi zimekuwa zikipungua. Walakini, wanasalia kukosoa sana kwenye mitandao ya kijamii kuhusu hali nchini Iran, watumiana video za maandamano. 

Hata hivyo Baghdad imetangaza siku ya Jumatano wito wa "haraka" wa balozi wa Iran kupinga mashambulizi hayo, diplomasia ya Iraq ikilaani "vitendo vya upande mmoja na vya uchochezi". Marekani "imelaani vikali" mashambulizi hayo, na kuionya Tehran dhidi ya mashambulizi zaidi dhidi ya makundi ya upinzani ya Wakurdi wa Iran. Berlin kwa upande wake ilishutumu "ongezeko lisilokubalika".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.