Pata taarifa kuu
HAKI-USALAMA

Iran: Makumi ya watu wauawa na mamia kukamatwa wakati wa maandamano

Idadi ya hivi punde ya waliofariki kutokana na maandamano nchini Iran imefikiwa watu 35, kulingana na vyombo vya habari vya serikali, 50 kulingana na shirika la upinzani la Iran Human Rights (IHR) lenye makao yake makuu Oslo. 

Maandamano huko Erbil, Kurdistan ya Iraq, mnamo Septemba 24, baada ya kifo cha mwanamke aliyekamatwa na jeshi la polisi la kuheshimisha maadili.
Maandamano huko Erbil, Kurdistan ya Iraq, mnamo Septemba 24, baada ya kifo cha mwanamke aliyekamatwa na jeshi la polisi la kuheshimisha maadili. REUTERS - AZAD LASHKARI
Matangazo ya kibiashara

Hasira hazipungui siku nane baada ya kifo cha Mahsa Amini, mwanamke mwenye umri wa miaka 22 aliyekamatwa na jeshi la polisi la kuheshimisha maadili kwa kuvaa hijabu vibaya. Ijumaa jioni, waandamanaji waliingia tena mitaani.

Video zinazorushwa kwenye mitandao ya kijamii hutufikia kutoka Iran, hata kama ni lazima zichukuliwe kwa tahadhari kwa sababu ni vigumu kuzithibitisha. Kila mara tunaona matukio yale yale: maandamano usiku, barabarani, na kauli mbiu zinazopinga serikali. Vijana wengi, wanawake wasiovaa hijabu, lakini pia wanaume. Shughuli za usafiri na biashara zimekwama, matairi au magari yanachomwa moto.

Na kisha kuna picha za ukandamizaji kitendo kinachoendeshwa na vikosi vya usalama. Kama vile video hii inayotangazwa sana na kuthibitishwa na shirika la habari la AFP, ambapo tunaona mwanamume aliyevalia sare ya polisi akielekeza silaha yake kwa waandamanaji na kuwapiga risasi, huko Shahre Rey, kusini mwa Tehran. Utawala umedhamiria kukomesha uasi, inazungumza wafanya ghasia, na njama zilizopangwa na Magharibi. Kaskazini mwa nchi, mkuu wa polisi wa jimbo la Guilan ametangaza kukamatwa kwa "wafanya ghasia 739, wakiwemo wanawake 60", kulingana na shirika la habari la Tasnim.

Siku ya Ijumaa, serikali iliandaa maandamano ya kupinga mandamano hayo watu weye hasira huko Tehran hasa ambapo mamia ya wanawake waliandamana kutetea uvaaji wa hijabu. Maandamano mengine yamepangwa kufanyika Jumapili alasiri.

Mamlaka pia zimepunguza utumiaji wa intaneti na mitandao ya kijamii, lakini hii haizuii kabisa Wairani kuendelea kutoa ushahidi. Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ), shirika la uangalizi wa vyombo vya habari lenye makao yake nchini Marekani, limesema waandishi wa habari 11 wamekamatwa nchini Iran tangu Jumatatu.

Kifo cha Mahsa Amini ndicho kilichochea maandamano haya. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 22 alikamatwa Septemba 13 huko Tehran kwa "kuvaa nguo zisizofaa" na jeshi la polisi la kuheshimisha maadili, linalohusika na kutekeleza kanuni kali za mavazi ya Jamhuri ya Kiislamu, na alifariki siku tatu baadaye.

Waziri wa Mambo ya Ndani amesema uchunguzi unaonyesha kuwa Mahsa Amini hakupigwa popote hali ambayo inadaiwa kuwa ilisababisha kifo chake wakati wa kukamatwa kwake, anaripoti mwandishi wetu wa Tehran, Siavosh Ghazi. Ameongeza kuwa vikwazo vilivyowekwa kwa watumiaji wa intaneti, na hasa kwenye Instagram na WhatsApp, vitadumishwa mradi maandamano yanaendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.